AIBU BOSI WA BANDARI AFUMWA AKILA URODA


Na Mwandishi Wetu
Ofisa Mwandamizi Uchukuzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Makao Makuu jijini Dar, Kitengo cha Makontena, Peter Milanzi (54) amejikuta ndani ya aibu nzito kufuatia madai kwamba, amekutwa akiwa na mke wa mtu kwenye nyumba ya kulala wageni ‘gesti hausi’, Ijumaa Wikienda linashuka na ‘diteilzi’. 

Tukio hilo lililoacha historia, lilijiri Desemba Mosi, 2010 (Siku ya Ukimwi Duniani) majira ya alasiri kwenye chumba namba tano cha hoteli moja (jina tunalo), Buguruni, Dar.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mume aliyejitambulisha kwa jina la Shaha Juma alidai kumbamba Milanzi akiwa na mkewe wa ndoa aitwaye Salia.

Chanzo hicho kikaongeza kudai kuwa, kabla ya fumanizi hilo lililokusanya mashuhuda kibao, mume wa mwanamke huyo alikuwa na kibarua kizito cha kufuatilia nyendo za ‘wezi’ hao mpaka ndani ya chumba hicho. Endelea kusoma habari hii...

AIBU BOSI WA BANDARI AFUMWA AKILA URODA

Na Mwandishi Wetu
Ofisa Mwandamizi Uchukuzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Makao Makuu jijini Dar, Kitengo cha Makontena, Peter Milanzi (54) amejikuta ndani ya aibu nzito kufuatia madai kwamba, amekutwa akiwa na mke wa mtu kwenye nyumba ya kulala wageni ‘gesti hausi’, Ijumaa Wikienda linashuka na ‘diteilzi’. 

Tukio hilo lililoacha historia, lilijiri Desemba Mosi, 2010 (Siku ya Ukimwi Duniani) majira ya alasiri kwenye chumba namba tano cha hoteli moja (jina tunalo), Buguruni, Dar.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mume aliyejitambulisha kwa jina la Shaha Juma alidai kumbamba Milanzi akiwa na mkewe wa ndoa aitwaye Salia.

Chanzo hicho kikaongeza kudai kuwa, kabla ya fumanizi hilo lililokusanya mashuhuda kibao, mume wa mwanamke huyo alikuwa na kibarua kizito cha kufuatilia nyendo za ‘wezi’ hao mpaka ndani ya chumba hicho.
“Unajua jamaa kabla hajawabamba, alifuatilia kwa karibu mno nyendo zao za siku hiyo mpaka wanaingia hapa gesti, pia akahakikisha anakijua na chumba,” kilisema chanzo hicho. 

Chanzo hicho kiliendelea kuanika kweupe kwamba, baada ya mwanaume huyo kujiridhisha kwamba, mkewe Salia na mzee huyo wamo ndani ya chumba hicho, aliita mashahidi ambao hawakutajwa majina ili kushuhudia tukio hilo.

Inadaiwa kuwa, mlango uligongwa na mume wa mwanamke huyo alizama ndani sanjari na mashahidi wake na kuanza kumhoji Bw. Milanzi kisa cha kuingia gesti na mke wa mtu ambapo alibabaika katika utetezi.

Lakini kwa upande wa pili, habari zilizopatikana kutoka kwa wahudumu wa gesti hiyo zinadai kwamba, Milanzi alijitetea kwa kusema kuwa, kama ni lawama basi mwanamke huyo ndiye anayetakiwa kubebeshwa, kwani hakuwahi kumwambia mzee huyo kuwa yeye ni mke wa mtu.

Aidha, ilisemekana kuwa, mbali na mwanamke huyo kutosema ni mke wa mtu, lakini pia hakuwa na dalili zozote zinazoonesha kuwa ameolewa, kama vile pete au hofu ya muda.
Ijumaa Wikienda lilimsaka Shaha na kumuuliza kama kuna ukweli wa madai hayo ambapo alikiri.

“Ni kweli, mke wangu nimemkuta chumba cha gesti na mwanaume, lakini nimeshawahi kumuonya kwa simu mara kadhaa huyu mzee aache kumchukua mke wangu, hakutaka kusikia,” alisema mume huyo.

Akaongeza: “Taarifa za tukio zipo Buguruni Polisi lakini RB ipo nyumbani (hakusema ni wapi) na kwa wakati huu siwezi kurudi kwa sababu nipo kazini.”

Wikienda lilipofika Kituo cha Polisi Buguruni, lilikosa ushirikiano kutoka kwa askari waliokuwa zamu siku ya Ijumaa baada ya kudai kuwa wao si wasemaji wa jeshi hilo.

Kwa upande wake, mzee Milanzi alipopatikana kwa simu yake ya mkononi siku ya Ijumaa alikiri kutokewa na tukio hilo, lakini akasema ‘amechoreshewa’.
“Ni kweli mkasa umenikuta, lakini umechezeshwa tu na watu. Yule mwanamke hajasema ameolewa,” alisema.

Mzee huyo aliongeza kuwa alipenda kufika kwenye ofisi za gazeti hili, Bamaga- Mwenge ili kuweka wazi kila kitu lakini akasema kwa bahati mbaya alikuwa safarini Morogoro. 

Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, dakika chache baada ya ‘mtuhumiwa’ huyo kumaliza kuongea utetezi wake, simu yake iliingia kwa mwandishi wetu ambapo sauti ya mtu mwingine ilisikika ikivurumisha matusi huku ikidai kama habari hii itatoka gazetini watu wataoneshana kazi mjini.

“Ninyi ni matepeli tu, hamna lolote, mnaunganisha unganisha picha halafu mnawasingizia watu, ala…(tusi), nakwambia hivi, ninyi…(tusi) kama hii habari itatoka basi hapa mjini (Dar) tutaoneshana kazi, si mnajifanya watoto wa mjini,” ilisema sauti hiyo na kukata simu.

Baada ya dakika tano, simu ya Milanzi iliingia tena kwa mwandishi na alipoipokea, sauti ya Milanzi ilisikika ikisema:

“Unajua bwana haya mambo yana utata mkubwa, mimi nimeonewa, hapa nilipo imebidi niwasiliane na watu wa Ikulu ili kuona tunafanyaje.”

Mwandishi wetu alimpa ‘kibali’ mzee huyo cha kuendelea kuwasiliana na watu wa Ikulu kama alivyodai lakini alimpa angalizo kuhusu watu wanaotumia simu yake kutukana na kukejeli.

KUKEMEA UOVU SI UDINI - PENGO



WAKATI serikali ikionyesha hofu ya udini kuingizwa kwenye siasa, Kanisa Katoliki limesema kuwa halitaacha kukemea uovu hata kama uovu na uozo huo unafanywa na watu walio madarakani kwa kuwa kufanya hivyo si udini.

Mara kadhaa wakati wa kampeni na baada ya kuapishwa Rais Kikwete alikuwa akizungumzia hofu yake ya udini kuingizwa kwenye siasa na akaweka bayana suala hilo wakati wa hotuba yake kwenye Bunge jipya, ingawa hakufafanua jinsi udini ulivyopenyezwa.

Lakini jana, askofu mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam, Polycap Kadinali Pengo alieleza kuwa hata kama walio kwenye mamlaka watawatishia, kanisa halitakuwa tayari kukaa kimya likiona kuna uovu.

Kardinali Pengo alitoa msimamo huo wa kanisa hilo kubwa nchini wakati akitoa mahubiri yaliyorushwa na kituo cha redio ya kanisa hilo cha Tumaini katika ibada iliyofanyika kwenye Kanisa la Utoto Mtakatifu kituo cha Hija kilichopo Pugu jijini Dar es Salaam.

Pengo alisema kuwa viongozi wa Kanisa Katoliki hawawezi kufumbia macho uovu kwa kuwa hata viongozi wa kanisa wanapofanya uovu hukemewa bila uoga.

"Kamwe kanisa haliwezi kufumbia macho uovu ili kundi moja liweze kukaa kwenye mamlaka na uovu wao. Hata kama mamlaka hiyo itatoa vitisho kwa viongozi wakuu, Kanisa Katoliki halitakaa kimya," alisema Pengo.

Alisema kuwa kukemea uovu kusionekane kuwa ni udini na ifahamike kuwa Kanisa Katoliki halimsimiki mtu awe rais, diwani au mbunge wa mahali popote, hivyo uovu wowote unaofanywa na mamlaka utaendelea kukemewa bila uoga.

"Katoliki linafahamu madhara yanayoweza kujitokeza katika jamii iwapo kanisa litampendekeza mtu kuwa kiongozi," alisema Pengo.

"Tuliombee taifa letu liepushwe na vitu vinavyotaka kuibuka katika taifa na kamwe kanisa haliwezi kumsimamisha mtu na kusema mumpigie kura," alisema.

Alisema hawawezi kuwanyamazia wanasiasa wakati hata maaskofu pia wanakemeana wanapotenda uovu.
"Uovu lazima ukemewe, si kitu ambacho mtu anafikiri kwamba mtu anaweza kutishia kwamba maaskofu wasikemee uovu," alisema Pengo.

Pengo alisema kuwa kutokana na kumbukumbu ya hapo zamani wakati wafalme walikuwa wakichaguliwa na mapadri na maaskofu, madhara yake yalijitokeza kwa kuwa jamii ilichaguliwa kiongozi asiyekubalika.

"Viongozi wa Katoliki wataendelea kukemea uovu huo kwa kuwa unaweza kusababisha mafarakano katika taifa linalotafuta ukweli na haki kwa ajili ya wote,"alisema Pengo.

Katika taifa lililo na watu takriba milioni 35 linaloundw ana idadi kubwa ya Wakristo na Waislamu wanaoshi pamoja, udini hauonekani kuwa silaha ya ushindi kwenye siasa.

Lakini suala hilo lilizungumzwa sana, hasa na viongozi wa chama tawala katika kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu, lakini hakuna aliyekuwa tayari kumnyooshea kidole mtu aliyekuwa akituhumiwa kutumia silaha hiyo ili ashinde.

Suspected Russian spy to be deported from UK


A Russian woman working for a member of the British Parliament has been detained on suspicion of espionage, the Sunday Times reported on Sunday. She is currently facing deportation.
25-year old Katia Zatuliveter, a researcher for Liberal Democrat MP Mike Hancock, was arrested at the request of MI5. The politician has denied knowing anything about Ms. Zatuliveter’s possible involvement in espionage.
“No-one has ever said to me under any circumstances whatsoever that she has been involved in anything like that,” the paper quotes Mr. Hancock as saying. “It is now in the hands of her lawyers. I am sure that in the end she will be proved to be right.”
Meanwhile, MI5 insists Ms. Zatuliveter deliberately sought a position with Mr. Hancock with intent to gain access to secret information. Mr. Hancock sits on parliament's defense select committee, which reviews defense policy.
“Her presence here is not considered to be conducive to national security. There was unhappiness about what she could have access to,” a source quoted by the paper states.

Mkapa ataka Katiba mpya • ASEMA NDIYO NJIA YA KUONDOA MIFARAKANO


RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, amevunja ukimya baada ya kusema ili kuzuia mifarakano ya kisiasa kwa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, zinahitaji kuwa na Katiba mpya, ikiwemo Tanzania.
Mkapa alisema hayo katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wanasheria wa jumuiya uliofanyika mjini Bujumbura nchini Burundi, mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya Rais Mkapa, iliyosomwa kwa niaba yake na Balozi Liberata Mulamula, njia pekee ya kuondokana na migogoro ya kisiasa kila nchi inapaswa kuwa na Katiba mpya ambayo itaainisha mambo yote ya msingi.

Alisema kama nchi wanachama zikiwa na Katiba mpya mambo mengi yanaweza kufanikiwa, lakini yameshindikana kutokana na nchi hizo kuendelea kutumia Katiba zilizorithi kutoka kwa wakoloni.

Alisema kumekuwa na malalamiko mengi kutokana na chaguzi nyingi toka kwa wanachama jinsi zinavyoendeshwa, huku shutuma na lawama nyingi zikielekezwa kwenye Katiba zilizopo.

Alisema Katiba zilizopo zimekuwa zikipendelea zaidi upande mmoja ambao unampa uhuru rais kuamua kila kitu.

Alisema uundwaji wa Katiba, lazima uendane na hali halisi, mahitaji ya kijiografia, kijamii na kisiasa. Endelea kusoma habari hii..
Image
Rais Jakaya Kikwete akipokea zawadi ya mchoro kutoka kwa Angela Kairuki, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kwa niaba ya akinamama wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), wakati wa hafla ya kumpongeza kwa ushindi mkubwa uliomwezesha kurejea madarakani baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu. Hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na mke wa Rais, Mama Salma Kikwete ilifanyika kwenye viwanja vya Biafra, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

NY would like WikiLeaks to find out about JFK, Elvis and 9/11

US returns stolen historical documents to Russia



US Immigration and Customs Enforcement (ICE) has handed over 21 historical documents that were reportedly stolen from Russia’s national archives between 1994 and 2002.
The documents range from the 18th to the 20th Centuries, and many of them were signed by Russian emperors and empresses. They were identified for sale or loan from several websites in the US. The ICE opened investigation after receiving a request from Russia’s watchdog of cultural heritage, Rosokhrankultura.
ICE director John Morton presented the documents to Russia’s ambassador Sergey Kislyak at a ceremony at the Russian Embassy in Washington DC.
“It is a great privilege and honor, on behalf of the United States, to return to the people of Russia a collection of historical documents that reflect their nation’s history and rich heritage,” Morton said.
ICE is the largest investigative arm of the Department of Homeland Security and deals with crimes involving the illicit importation and distribution of cultural property. Its task is to investigate and eventually return art and items of cultural significance to their countries of origin and rightful owners.

Kanisa Katoliki lawatenga wanachama 400 wa CCM

KATIKA kile kinachoonekana kuithibitishia jamii kuwa nyumba za ibada si mahala pa siasa, Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga limewafukuza na kuwazuia kushiriki shughuli za kanisa zaidi ya waumini wake 400 wanaotuhumiwa kuisaliti imani ya kanisa hilo kwa kukishabikia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni.

Miongoni mwa waumini wanaotajwa kuwa wamesimamishwa na kanisa hilo ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Hipolitus Matete na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Sumbawanga, Charles Kabanga.

Habari za uhakika ambazo HABARILEO Jumapili imezipata zinasema kwamba, uamuzi huo wa kanisa umelenga kujisafisha na 'kashfa’ ya kuegemea upande fulani wakati wa kampeni na baadaye uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.

Chanzo chetu cha habari kimepasha kwamba, wanaCCM hao wanaotuhumiwa na kanisa hilo wanahusika kufanya mikutano ya ndani, kuvaa sare za chama hicho na kumshabikia waziwazi aliyekuwa mgombea wa Ubunge kupitia CCM katika Jimbo la Sumbawanga Mjini,
Aeshi Hilaly.

Kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu huo mgombea ubunge wa CCM, Aeshi aliibuka kidedea kwa kutangazwa mshindi dhidi ya mgombea wa Chadema, Norbet Yamsebo ambaye kwa sasa amekata rufaa Mahakama Kuu mjini hapa kupinga matokeo hayo.

Inaelezwa kwamba, mgogoro wa kiimani baina ya Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga Mjini na waumini wake ambao ni wanaCCM, umetokana na waumini hao kupuuzia agizo la kanisa la kutomshabikia Aeshi kwa madai kwamba, alikufuru imani ya kanisa hilo kwa kujifananisha na Mwana wa Mungu, Yesu Kristu.

Baadhi ya viongozi wa kanisa jimboni humo wamekuwa wakimtuhumu mgombea huyo wa CCM pale alipodai katika moja ya mikutano yake ya kampeni kwa kufananisha mafiga matatu na Utatu Mtakatifu ambao mgombea huyo anadai kuwa alikufuru imani hiyo kwa kumfananisha mgombea Urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kama Mungu Baba, mgombea ubunge kama Yesu Kristu mwana wa Mungu na wagombea Udiwani sawa na
Roho Mtakatifu.

Katibu wa CCM Mkoa wa Rukwa, Kapteni Fratern Kiwango amethibitisha kutengwa kwa wanachama wa chama hicho ambao ni waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga.

“Ni kweli hadi sasa kanisa hilo limewafukuza na kuwazuia wanaCCM zaidi ya 400 kupokea sakramenti zozote kwenye Kanisa Katoliki la hapa,” alisema Kapteni Kiwango aliyewataja baadhi ya waliofukuzwa na kusimamishwa kuhudhuria ibada za misa takatifu kuwa ni pamoja na Matete, Kabanga, dereva wa Katibu wa CCM mkoa wa Rukwa aitwaye Vitalis Kalwangwa na mkewe na Katibu Mwenezi wa CCM Tawi la Majengo, Christina Tinde.

Inadaiwa kuwa waumini hao ni kutoka kanisa la Familia Takatifu lililopo Chanji mengine ni Kristu Mfalme , Katandala na Kanisa la Kiaskofu lililopo Mazwi mjini hapa ambapo kanisa lililopo kijiji cha Mlanda limefungwa na waumini wake wote wamezuiwa kupata
huduma yoyote ya kiroho kwenye kanisa hilo.

Inadaiwa kuwa pamoja na kuzuiwa kuingia makanisani na kuhudhuria ibada ya misa takatifu waumini hao wamezuiwa pia kupokea sakramenti zozote katika Kanisa Katoliki.

Pia wamezuiwa kupata huduma za kiroho kanisani zikiwemo kufunga ndoa, kubatizwa au kupata kipaimara na pia kufanyiwa ibada wakati wa maziko hadi hapo suala lao litakapopatiwa ufumbuzi ambapo itategemewa zaidi jitihada zao binafsi na huruma ya Mungu.

Mwandishi wa habari hizi alisoma baadhi ya nakala za barua za kuwasimamisha kupokea sakramenti kwenye kanisa hilo zilizosainiwa na Paroko wa Kanisa la Kristu Mfalme, Padri Pambo Mlongwa.

Sehemu ya barua hiyo inasema; "Kufuatia mwenendo mbovu wakati wa uchaguzi mkuu, huku ukiendekeza vitendo vya rushwa na usaliti wa imani Katoliki.

“Kwa heshima ya Mungu wetu na utatu mtakatifu wa kanisa, Mama kanisa Mtakatifu kwa nguvu ya Sheria ya kanisa CIC 13669, CIC1389,CIC 13712 na CIC 1391 naagiza usipokee sakramenti zozote katika Kanisa Katoliki… tekeleza amri hii mara umalizapo kuisoma barua hii.”

Padri Pambo alipohojiwa kwa njia ya simu ili kupata ufafanuzi zaidi wa suala hilo alisema kwamba, yuko mbali sana ambako hataki mtu yeyoye ajue aliko.

"Sawa mimi ni kiongozi wa kiroho kwa sasa sitaki kabisa mtu yeyote hata wewe ujue wapi nilipo, niko mbali sana kwa sasa nakushauri nenda ofisini ni suala la kiofisi hilo kwa sasa sina majibu yake,” alisema kiongozi huyo wa kiroho.

Lakini kabla ya mawasiliano ya siku hiyo, kwa nyakati tofauti Padri Pambo alipokuwa
akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu alikiri kuwa mgombea wa CCM, Aeshi alikuwa amekufuru imani na Kanisa Katoliki kwa kujifananisha na Yesu Kristu Mungu Mwana ambapo Kanisa liliwasilisha malalamiko yake kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuja mjini hapa kumnadi mgombea huyo, lakini hawakuweza kufikia mwafaka.

Pia zimekuwa taarifa mjini hapa kwa Padri Pambo amekimbia kanisa lake la Kristu Mfalme kwa kile kinachodaiwa kuwa amekwenda kujificha kusikojulikana ili kukwepa hasira za waumini wa kanisa hilo wanaopinga kufukuzwa kwa wenzao kwa sababu ya itikadi zao za kisiasa.

Naye Paroko wa Kanisa la Kiaskofu mjini Sumbawanga, Padri Deo Simemba hivi karibuni alipohojiwa na gazeti hili alikiri kuwa kanisa limeanza kuwasimamisha baadhi ya waumini wake kwa kile alichodai kuisaliti imani ya Kanisa Katoliki.

Kutokana na tukio hilo, Katibu wa CCM wa Mkoa amelitahadharisha kanisa hilo kwa kujiingiza kwenye malumbano ya kisiasa.

Baadaye, gazeti hili liliwasiliana na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Anthony Makunde ili aweze kulizungumzia suala hilo na alipopatikana kwa njia ya simu alisema:

“Kwa nafasi yangu, naweza kusema sijui lolote kwa sababu sijapata taarifa rasmi na inawezekana kwa kuwa katika siku za hivi karibuni nilikuwa na vikao vingi pamoja na kuhudhuria mafahali pale Chuo Kikuu cha Madaktari Bugando (Mwanza).”

When will democracy come to Africa?

Wagombea wote waapishwa urais Ivory Coast

Ivory Coast iko katika janga kubwa la kisiasa, baada wa wagombea wote wawili wa urais kujiapisha kuongoza nchi.
Gbagbo
Laurent Gbagbo akila kiapo
Rais anayetetea kiti chake Laurent Gbagbo amekula kiapo cha kuongoza muhula mpya, lakini saa kadhaa baadaye Alassane Ouattara pia akala kiapo.
Marekani, Umoja wa Mataifa na Ufaransa zimesema Bw Ouattara ndiye ameshinda uchaguzi huo.
Bw Ouattara alitanagzwa mshindi la Tume ya Uchaguzi, lakini matokeo hayo yalitenguliwa na Baraza la Katiba, ambalo linaongozwa na mshirika wa Bw Gbagbo.
Uchaguzi wa raindi ya pili ya urais, ulikuwa na lengo la kuliunganisha taifa hilo ambalo ndio mzalishaji mkubwa zaidi ya kakao duniani, baada ua kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002. Endelea kusoma habari hii

Pinda akataa shangingi



WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameonyesha kwa vitendo kuwa yeye ni mtoto wa mkulima baada ya kukataa gari jipya ka kifahari alilonunuliwa na wasaidizi wake kwa akisema kwamba alilonalo linamtosha.


Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana jioni kwa njia ya simu, Pinda alisema kuwa uamuzi huo aliuchukua mwaka huu kabla ya uchaguzi mkuu kuanza baada ya kukataa kulitumia gari jipya aina ya Landcruiser VX 8 lenye thmamani ya sh milioni 280.

Alisema kuwa aliamua kukata kulitumia gari hilo baada ya kungundua kuwa alilonalo ambalo ni la bei ndogo kuliko hiyo bado lina uwezo.

"Ni kweli nimelikataa kulitumia gari hilo kwani niliona hata gari hili ambalo nimeanza nalo kulitumia kama mawaziri mkuu bado halikuwa na matatizo, sasa kwa nini nipewe jingine jipya, hii itakuwa ni matumizi mabaya fedha za serikali," alisema.

Alisema baada ya kulikataa kulitumia gari hilo aliwaagiza watalaam wake kwa sababu tayari walishalinunua kumtafuta mtu mwingine wa kumpa kulitumia, lakini kama angeshirikishwa katika mchakato wa awali hangewakubalia.

Pinda aliteuliwa kuwa Maziri Mkuu mwaka 2008 baada ya aliyekuwa akishika wadhifa huo, Edward Lowassa kujiuzulu kutokana na kuibuka kwa kashfa ya Richmond pamoja na mawaziri wengine ambao Ibrahim Msabaha aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Nazir Kamaragi aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Pinda ambaye anakuwa Waziri Mkuu wa kwanza kukataa gari jipya alilonunuliwa kwa lengo la kubana matumizi alisema kuwa watu wanatakiwa kujua kuwa Tanzania nchi masikini sana hivyo tunahitaji kutumia vyema kipato chetu badala ya kukitumia kwa matumizi ambayo sio ya lazima.

Alisema kuwa mazoea ambayo Watanzania wajijengea kwamba viongozi wa juu wa serikali wanapenda kila mara vitu vipya na vya gharama kubwa hanapaswa kufutwa kwa vitendo.

"Hii tabia ya kufikiri kwamba gari zuri lazima liendane na hadhi ya mtu ni vyema sasa tukaiacha," alisema na kuongeza:

"Kutokana na tabia hii hata watengenezaji wa magari nao wamejua udhaifu wetu wamekuwa wakijaribu kubadilisha muundo kidogo tu na kuja na magari mpya ambayo wanayauza kwa bei kubwa".

Pinda ambaye ndiye anayetoa kibali cha ununuzi wa magari ya serikali alisema hatakubali kuidhinisha viongozi wa serikali kutaka kununua magari ya kifahari wakati wanaweza kutumia magari ya kawaida.

Hata hivyo,alisema kuwa hawezi kupiga marufuku moja moja ununuzi wa magari ya kifahari kwa vile ni jambo ambalo linahitaji kuchukuliwa kwa hatua, lakini taratibu watedaji wa serikali watahamia katika kutumia magari ya kawaida.

Waziri Mkuu ambaye akiwashukuru wabunge kwa kumwidhisha kuwa waziri mkuu alisema yeye ni mtoto wa mkulima, alisema suala la kudhibiti ununuzi wa magari ya fahari kwa viongozi wa serikali alishaalianza muda mrefu.

Mwaka jana Pinda, aliwaagiza watendaji wa serikali watafute namna ya kupunguza matumizi ya fedha za umma ikiwa ni pamoja na kutonunua magari ya kifahari.

Aliwataka watendaji hao wabadilike, waache ubinafsi na wasijifikirie wao tu, kuna mamilioni ya watanzania wanaohitaji fedha kidogo zilizopo.

Katika Wizara za Serikali kuna magari mengi ya aina ya Toyota Land Cruiser VX yanayouzwa kati ya Sh 160 milioni hadi Mwaka 2008 serikali chini ya uongozi wa Pinda ilifanya marekebisho makubwa ya namna ya udhibiti wa uendeshaji wa magari ya kifahari kwa mawaziri na viongozi wengine ili kuondokana na matumizi mabaya ya mali za umma.

Ripoti ya Mpango wa Serikali kuhusu Orodha ya Magari yake na Kudhibiti Matumizi ambayo ilipendekeza pamoja na mambo mengine magari ya kifahari ya mawaziri maarufu kama mashangingi yanunuliwe kila baada ya miaka saba badala ya miwili ya wakati huo.

Utaratibu uliozoeleka ni kwamba, gari la waziri huweza kununuliwa kila baada ya miaka miwili tangu linunuliwe na kuanza kutumika, kisha hutumiwa na watendaji wa ngazi ya chini, au kuuzwa au waziri 'kujiuzia'.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya serikali ya mwezi Aprili 2008 jumla ya magari yote ya serikali nchini yalibainika ni kati ya 35,000 hadi 40,000.

Kati ya orodha hiyo magari ya kifahari ya Toyota Landcruiser Vx8 na VX, Gx na aina nyingine ya Landcruiser yalikuwa kati ya 10,000 hadi 15,000.

Takwimu za sasa, gari moja aina Toyota VX8 linauzwa kwa sh 280 na kwamba VX la kawaida ni sh 120 milioni, huku gharama za operesheni ikiwa ni pamoja na matengenezo ya kila wiki na mafuta ni kati ya Sh moja hadi 1.5 milioni, kutegemea safari.

Magari hayo 40,000 ni kuanzia Serikali Kuu na Halmashauri za Wilaya, miji, manispaa na majiji, ambayo ni pamoja na yale ya miradi maarufu kama DFP ambayo hutokana na wafadhili.

Orodha hiyo inaonyesha sehemu kubwa ya magari hayo ni Toyota Pickup na Hard Top, ambazo zimekuwa zikitumika zaidi vijijini huku mashangingi ya Vx na Gx yakirandaranda mijini.

Pendekezo la serikali ni kwamba katika ngazi ya Serikali za Mitaa, linataka Mkuu wa Mkoa pekee ndiye atumie Vx ili kuwezesha Rais anapofika aweze kulitumia huku Wakuu wa Wilaya na watendaji wengine wakitakiwa kupatiwa gari za kawaida kama Toyota Landcruiser si Vx.

Magufuli, Mwakyembe hatarini

MIKAKATI ya kuwakwamisha kiutendaji Waziri wa Ujenzi, John Magufuli na Naibu wake, Dk. Harrison Mwekyembe, inadaiwa kuanza kuandaliwa na vigogo wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kushirikiana na baadhi ya makandarasi, Tanzania Daima Jumapili imedokezwa.

Mawaziri hao wameanza kuonekana tishio kwa baadhi ya vigogo wa TANROADS ambao inadaiwa walikuwa wakijinufaisha kupitia zabuni mbalimbali zilizokuwa zikitangazwa na serikali.

Vigogo hao wa TANROADS inadaiwa walikuwa wakivuna fedha kutoka kwa wamiliki wa kampuni za ujenzi ambao walikuwa wakitoa fedha ili kujenga ushawishi wa kampuni zao kupewa ushindi wa zabuni husika.

Tanzania Daima Jumapili imedokezwa kuwa hivi sasa baadhi ya vigogo hao wamekuwa na wasiwasi wa kuendelea na mchezo huo wa kuvuna fedha hasa baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua Magufuli kuwa Waziri na Dk. Mwakyembe kuwa Naibu Waziri.

Magufuli alipoanza kazi katika wizara hiyo alibatilisha tangazo la ajira lililotolewa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANROADS, Ephraim Mrema, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akishtumiwa kwa kuiendesha ofisi hiyo kwa masilahi ya kundi fulani la watu.

Kinachochangia wasiwasi wa watendaji hao ni hatua ya wizara hiyo kutoa taarifa kuwa imempa barua ya kuondoka kazini Mkurugenzi wa TANROADS, Ephraim Mrema, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akituhumiwa kuitumia ofisi hiyo kwa masilahi binafsi.

Mrema, pia alikuwa akidaiwa kufanya marekebisho kwa baadhi ya watendaji mikoani na makao makuu kwa lengo kuweka safu mpya itakayokuwa na utii kwa yale atakayokuwa anawaagiza.

Marekebisho hayo yalizusha mzozo mkubwa ambao ulitikisa TANROADS na Wizara ya Miundombinu iliyokuwa ikiongozwa na Dk. Shukuru Kawambwa ambaye kila mabadiliko yanayofanywa na Rais Jakaya Kikwete katika baraza la mawaziri humkumba.

Tanzania Daima Jumapili imedokezwa kuwa baadhi ya makandarasi ambao walikuwa wakinufaika na kuwapo kwa Mrema hivi sasa wanafanya mikakati ya chini kwa chini ikiwamo kuhujumu baadhi ya miradi ili uongozi wa Mafuguli uonekane haufai, hasa katika sekta ya ujenzi wa barabara.

Habari hizo zilidokeza pia kuwa Mrema, alikuwa akiungwa mkono na baadhi ya vigogo waliopo serikalini ambao wana kampuni za ujenzi lakini wamekuwa wakiwatumia ndugu au jamaa zao kuziendesha.

Tanzania Daima Jumapili, ilidokezwa pia kuwa Mrema alikuwa na uhusiano na baadhi ya vigogo wa ikulu au familia zao jambo lililokuwa likichangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa ushirikiano na wafanyakazi wenzake.

Taarifa hizo zilidai Waziri Magufuli, anaonekana kuwa tishio kwa makandarasi wa barabara ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakinufaika na fedha za ujenzi wa barabara, ambapo walikuwa wakizidisha gharama zake.

Wakati wa utawala wa Magufuli katika wizara hiyo, ujenzi wa kilometa moja ya lami ilikuwa sh milioni 300-400 lakini hivi sasa kilometa moja ni sh bilioni moja.

Wataalamu wa masuala ya ujenzi wanabainisha kuwa pamoja na kupanda kwa gharama za vifaa, lakini gharama za ujenzi wa kilometa moja ya lami kwa sh bilioni moja ni mkubwa na kuna uwezekano baadhi ya watendaji na makandarasi wananufaika na ongezeko hilo.

Wataalamu hao wanadokeza kuwa Magufuli atakabiliwa na wakati mgumu wa kurekebisha jambo hilo ambalo kwa kiasi kikubwa linawanufaisha makandarasi na wale wanaofanikisha mipango ya kuwapatia zabuni.

Ufuatiliaji wa karibu wa Magufuli pamoja na uwezo wake wa kuhifadhi takwimu ndio unaowatia hofu wale wote waliokuwa wakinufaika na fedha za serikali kwa kutumia njia za mkato.

Historia ya Magufuli kufuatilia ubora wa barabara au jengo linalojengwa ndio unaozidisha hofu kwa makandarasi ambao wamekuwa wakijenga chini ya viwango kwa lengo la kujinufaisha zaidi.

Mara kadhaa wakati akiwa Waziri wa Ujenzi, Magufuli alikuwa akiyakataa majengo, barabara au kuvunja mikataba pale anapoona havikujengwa kwa kiwango kinachotakiwa.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili kuhusu kuwapo kwa taarifa hizo za kuhujumiwa, Mwakyembe alisema ni mapema mno kulizungumzia jambo hilo, kwa sababu ndiyo kwanza ameingia ofisini na anahitaji muda zaidi kujua nini kinafanyika ndani na nje ya ofisi hiyo.

Alisema kuwa muda ndio utakaoamua kuhusu njama hizo, lakini katika mazingira ya kawaida hakuna mkandarasi au mtendaji wa serikali ambaye anaweza kufanikisha hujuma kubwa kama hiyo.

“Ndugu yangu, sina jibu la kukupa kuhusu njama hizo, lakini ni vema tukapeana muda ili tuweze kufanya kazi,” alisema Mwakyembe.

Google apologizes for mixing up Russian flag colors

Google has apologized for a mistake in their logo, dedicated to Russia’s victory in the bidding for World Cup 2018.
The logo on Google‘s front page, published on the night of December 2, had the colors of the Russian flag all mixed up, with the blue and the red stripes in their opposite places.
"We apologize for a mistake we made in our logo last night. We’re trying to fix it as quickly as possible. Hope you like the logo," the statement in the official Google Russia microblog on Twitter said.
The logo was corrected a few hours after the apologies appeared on the web.
The flag of the Russian federation is a tricolor of three equal horizontal stripes – white on the top, blue in the middle and red on the bottom.
Russia has won the honor of hosting the World Cup 2018 after a December 2 vote by the FIFA executive committee.

Upinzani washika hatamu Ivory Coast

Upinzani "Washinda" urais Ivory Coast

Tume ya uchaguzi wa Ivory Coast imesema mgombea urais wa upinzani Alassane Ouattara ameshinda uchaguzi wa raundi ya pili ya urais, ingawa mahakama ya katiba imepinga matokeo hayo.
Ouattara
Alassane Ouattara
Mwandishi wa BBC John James aliyepo mjini Abidjan amesema kutakuwa na mvutano kati ya taaisisi hizo mbili huku matokeo yake yakiwa hayajulikani.
Wafuasi wa rais Laurent Gbagbo walijaribu kupinga matokeo hayo, wakisema kumekuwa na wizi upande wa kaskazini.
Eneo hilo bado limesalia chini ya udhibiti wa waasi wa zamani, anao ambalo Bw Ouattara ana umaarufu mkubwa. Soma habari kamili

Upinzani "Washinda" urais Ivory Coast

Tume ya uchaguzi wa Ivory Coast imesema mgombea urais wa upinzani Alassane Ouattara ameshinda uchaguzi wa raundi ya pili ya urais, ingawa mahakama ya katiba imepinga matokeo hayo.
Ouattara
Alassane Ouattara
Mwandishi wa BBC John James aliyepo mjini Abidjan amesema kutakuwa na mvutano kati ya taaisisi hizo mbili huku matokeo yake yakiwa hayajulikani.
Wafuasi wa rais Laurent Gbagbo walijaribu kupinga matokeo hayo, wakisema kumekuwa na wizi upande wa kaskazini.
Eneo hilo bado limesalia chini ya udhibiti wa waasi wa zamani, anao ambalo Bw Ouattara ana umaarufu mkubwa.
Gbagbo
Laurent Gbagbo
Uchaguzi huu una lengo la kuiunganisha nchi hiyo ambayo huzalisha kakao kwa wingi zaidi duniani.
Matokeo ya mchuano wa raundi ya pili uliofanyika siku ya Jumapili, yamecheleweshwa sana na kusababisha hali ya wasiwasi nchini humo.
G na O
Laurent Gbagbo (kushoto) na Alassane Ouattara (kulia)
Watu wasiopungua waliuawa siku ya Jumatano usiku katika shambulio kwenye ofisi ya chama cha Bw Ouattara.
Mahakama ya Katiba imesema tume ya uchaguzi kushindwa kutangaza matokeo siku ya Jumatano ina maanisha taasisi hiyi sasa inachukua majukumu.
lakini wakati huohuo tume ya uchaguzi imesema Bw Ouattara ameshinda kwa asilimia 54 ya kura.

Genge la Mafia 'la tawala' Urusi


Vladimir Putin
Jaji huyo anadai kuwa Vladimir Putin anauhusiano na genge la mafia.
Taarifa za hivi karibuni zilizochapishwa na mtandao wa Wikileaks, zinamnukuu mwendesha mashataka mmoja kutoka Uhispania akisema kuwa serikali ya Urusi inaendeshwa na genge la mafia.
Jaji Jose "Pepe" Grinda Gonzales alielezea ubalozi wa Marekani mjini Madrid kuwa hali hiyo pia inashuhudiwa nchini Belarus and Chechnya.
Mawasiliano hayo yaliochapishwa na gazeti la The Guardian yanamnukuu akisema kuwa ni vigumu kutofautisha mikakati ya serikali katika nchi hizo na ile ya magenge hayo ya mafia.
Jaji Gonzales ambaye pia aliongoza uchunguzi kuhusu harakati za kundi la mafia kutoka Urusi nchi mwake, pia anahoji ikiwa Waziri Mkuu Vladimir Putin anashirikiana na kundi hilo.
Mtandao wa Wikileaks umekuwa ukifichua maelfu ya nyaraka za siri za mawasiliano kati ya mabalozi wa Marekani kuhusu viongozi wa nchi wanazowakilisha.
Serikali ya Marekani imeomba radhi kufuatia ufichuzi huo.
Rais Barack Obama amemteua Russell Travers, mtalaamu wa masuala ya Ugaidi kuchunguza jinsi Wikileaks ilivyopata nyaraka hizo na kuimarisha usalama kwenye mtandao wa mawasiliano ya serikali.

Mawakili wampinga Dk Shein kuteua majaji

CHAMA Cha Mawakili Zanzibar (ZLS) kimepinga uteuzi wa majaji wa Mahakama Kuu uliofanywa na Rais wa Zanzibar (SMZ), Dk Ali Mohammed Shein Novemba 29 mwaka huu wa 2010 na kuhoji uhalali wa uwepo wa Jaji Mkuu wa Zanzibar aliyestaafu.

Tayari ZLS kimemwandikia barua Dk Shein Novemba 30, ambayo Mwananchi ilifanikiwa kuiona nakala yake kikieleleza kuwa hakijaridhishwa na uteuzi huo kwa kuwa haukuzingatia vigezo na kwamba, umekiuka sheria kwa kuwa hakijashirikishwa.

Barua hiyo ya ZLS ya Novemba 30, mwaka huu yenye kumbukumbu namba ZLS/IKULU/001 tayari imepelekewa Dk Shein ikiwa na saini ya Rais wa chama hicho, Yahya Khamis Hamad na mawakili 15 kwa niaba na wenzao zaidi ya 50, kupinga uteuzi huo wa majaji uliofanywa na Rais Dk Shein.

Novemba 29, mwaka huu Rais wa Zanzibar kwa mamlaka aliyopewa na katiba ya SMZ aliteua majaji wanne wa Mahakama Kuu pamoja na Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi, Haroub Sheikh Pandu.

Majaji wanne walioteuliwani Abdul-hakim Ameir Issa, Fatma Hamid Mahmoud, Mkusa Isaac Sepetu na Rabia Hussein Mohammed.

"Rais, katika uteuzi wako huo, ambao umetumia mamlaka uliyopewa na Katiba ya Zanzibar ya 1984 kifungu cha 94(2) na (3), Chama cha Mawakili hakina mashaka na uteuzi wa Abdul-hakim Ameir Issa, wala uteuzi wa Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi, Haroub Shehe Pandu. Mashaka yetu yapo katika uteuzi wa waheshimiwa kuanzia nambari 2 mpaka 4,” Sehemu yabarua yao kwa Dk Shein ZLS inasomeka:

Hata hivyo, ZLS ilisema Rais hawezi kuwaelewa majaji wala hakuna sababu ya kumjua yeyote kati ya majaji wanne aliowateua, lakini wanachoamini uteuzi wake unatokana na ushauri uliopewa na Tume ya Utumishi ya Mahakama iliyoanzishwa chini ya Sheria Namba 13 ya mwaka 2003 ambayo Mwenyekiti wake ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid pamoja na wasaidizi wa rais wengine katika sekta ya sheria.

“Rais, sisi mawakili ambao tumetia saini barua hii tukiwa ni wadau wakubwa katika sekta hii, tuna imani kubwa nawe ..., lakini tunaamini washauri wako hawakukutendea haki walipokushauri uwateue Fatma, Mkusa na Rabia kuwa majaji wa Mahakama Kuu,” ilieleza barua ya ZLS na kuongeza:

"Rais, haitoshi tu kusema kwamba Jaji Mteule ametimiza masharti ya Katiba na hivyo anafaa kuwa Jaji wa Mahkama Kuu.

Vipo vigezo vyengine ambavyo ni lazima viangaliwe kabla ya uteuzi wa jaji wa Mahakama Kuu kufanyika. Nafasi ya ujaji ni nafasi ya juu kabisa katika ngazi ya mahakama zetu na pia ni nyeti. Utaalamu uliobobea, rekodi iliyothibitika, umakini wa hali ya juu, kujiamini, uadilifu na umahiri wa hali ya juu - vyote kwa pamoja vinahitajika.”

Mawakilili hao walisema kuwa kifungu cha 94(2) cha Katiba kinasema kuwa Majaji wa Mahakama Kuu watateuliwa na Rais kutokana na mapendekezo ya Tume ya Utumishi ya Mahakama wakati.

“Rais, Chama cha Mawakili kina mjumbe katika Tume ya Utumishi ya mahakama. Pia wajumbe wengine wa tume ni watu walio karibu na Chama cha Mawakili. Tunapenda kukuthibitishia kwamba, hakuna kikao chochote cha Tume hiyo ambacho kimemjadili Rabia Hussein. Hivyo uteuzi wake umefanywa kinyume kabisa na Katiba ya Zanzibar na hauwezi kusimama katika macho ya sheria,” walisema mawakili hao na kuongeza:


“Wateule wa ujaji tuliowataja hapo juu, hawatokuwa majaji rasmi, kikatiba na kuanza kazi ya ujaji wa Mahakama Kuu, mpaka baada ya kula kiapo. Hilo likishafanyika, itakuwa dhiki sana kutenugua uteuzi huo. Hivyo, tunakuomba Mheshimiwa Rais, utafakari upya juu ya uteuzi huo na uridhike kuusitisha,” walisema mawakili hao.

Mmoja wa majaji hao wanne waliolalamikiwa (Fatma Hamid Mahmoud) ametajwa kuwa ni mtoto wa Jaji Mkuu wa Zanzibar Hamid Mahmoud huku mawakili hao wakieleza pia kwamba uwepo wake katika wadhifa wa jaji mkuu una mashaka kikatiba na ukiukwaji wa taratibu za kisheria.

“Mheshimiwa Rais, sisi kama chama cha mawakili, tunaamini hata uwepo wa Hamid Mahmoud kama Jaji Mkuu wa Zanzibar una mashaka tele ya kikatiba. Inaeleweka kwamba Hamid Mahmoud alistaafu kwa hiari alipotimiza miaka 60," imeeleza barua ya ZLS na kuongeza:

"Kama alitakiwa kuendelea kushika wadhifa huo, alipaswa kwanza kupewa mkataba wa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Mkataba wa aina hiyo ulilazimu kujadiliwa na Tume ya Utumishi ya Mahakama kwa mujibu wa kifungu cha 95 (1) cha Katiba ambacho kinasema: "Bila ya kuathiri masharti ya kifungu hiki, Jaji wa Mahakama Kuu ataendelea kushika wadhifa wake hadi kufikia umri wa miaka 60 ambapo anaweza kustaafu kwa hiari ama kuendelea hadi kufikia umri wa miaka 65 ambapo atastaafu kwa lazima.


Aidha (2) Bila ya kuathiri masharti ya kijifungu cha (1) cha kifungu hiki, Rais kwa kushauriana na Tume ya Utumishi ya Mahkama anaweza kumteua tena Jaji aliekwisha staafu kushika madaraka ya Jaji wa Mahkama Kuu kwa muda au kwa ajili ya kesi maalum.


Kutokana na maelezo hayo ZLS walisema kuwa hakukuwa na sababu yoyote kuendelea jaji mkuu huyo kuendelea kufanya kazi katika mkataba kwa kuwa Katiba ilikuwa inamruhusu kuendelea na ajira hadi kufikia miaka 65".

Barua ianeleza kuwa kama Jaji Mkuu alitakiwa kuendelea na nafasi yake baada ya kumaliza utumishi wake, ililazimu mambo mbalimbali kufuatwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar (kifungu cha 94(1), 94(2), 94(6)(a) na (b).

Waliyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na kuwa ateuliwe kuwa Jaji wa Mahkama Kuu, Mapendekezo ya uteuzi wake yatokane na Tume ya Utumishi ya Mahkama; Endapo ni Jaji wa Mkataba, “masharti ya kazi, marupurupu na kiinua mgongo cha jaji wa mkataba wa kipindi maalum yataamuliwa na Tume ya Utumishi ya Mahkama.
Wameleeza katika barua hiyo kuwa kifinga cha 94(6)(b) kinasema iwapo atateuliwa kuwa jaji basi atakula kiapo cha Jaji wa Mahkama Kuu.

“Kuendelea kwake kuwa Jaji Mkuu kunakuwa na mashaka ya kikatiba na sisi tusingependa nchi yetu iwe na Jaji Mkuu ambaye uteuzi wake umegubikwa na kasoro kadhaa za kikatiba,” ilieleza ZLS.

Kwa mujibu wa ZLS, suala la kuwa jaji au Jaji Mkuu wa mkataba linalopigwa vita katika Mahakama za Jumuiya ya Madola kwa sababu mikataba inaondoa kinga ya kikatiba aliyonayo Jaji wa Mahkama Kuu, hivyo kudumaza uhuru wa Mahakama na kwamba, jaji wa mkataba hawezi kufanya kazi yake bila ya hofu wala woga kwa mamlaka ya uteuzi.

Hata hivyo ZLS ilisema kuwa haihoji mamlaka ya rais kikatiba bali wanatoa tahadhari kwake kama mchango wao katika kujenga mahakama iliyotukuka, hasa kutokana na wananchi kupoteza imani kwa mahakama ziliopo sasa hivyo ni vyema kuepuka mambo yanayoonekana dhahiri kulenga katika kudumaza ufanisi wa mahakama katika suala la utoaji haki.

Nakala ya barua hiyo imepelekwa kwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Jaji Mkuu waTanzania; Jaji Mkuu wa Zanzibar; Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar; Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Zanzibar; Mwanasheria Mkuu waTanzania; Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar; Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai.

Magufuli amfuta kazi mkuu wa TANROADS

HATIMAYE Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Ephraim Mrema, ameong’olewa rasmi katika nafasi hiyo na kukabidhi ofisi hiyo jana kwa Kaimu Mtendaji aliyeteuliwa, Injinia Patrick Mfugale.

Mwanzoni mwa wiki hii Waziri mpya wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alimtaka Mrema afanye kazi huku akiamini haondoki katika wadhifa huo na aweke matumaini ya kuishi kwa miaka 100.

Kwa kirefu Mrema amekuwa akiandamwa na tuhuma mbalimbali za kifisadi katika wakala huo, ikiwa ni pamoja na kudaiwa kuvunja mikataba na makandarasi bila kufuata taratibu.

Hata hivyo, taarifa za kuaminika ambazo Tanzania Daima inazo kutoka TANROADS, zilieleza kuwa uamuzi huo ulifikiwa jana baada ya viongozi wakuu wa wizara hiyo kukutana na kujadili juu ya suala la Mrema na kufikia hatua ya kumuengua.

“Huu uamuzi umefikiwa leo na viongozi wetu wakuu, kwa kweli tumefurahishwa sana maana ukiangalia kwa kipindi chote alichokaa katika uongozi wake Wakala huu umepoteza sifa, huku akivunja mikataba kila mara ya makandarasi bila kufuata utaratibu,” alisema mtoa taarifa wetu.

Alisema kuwa Mrema hajafurahishwa na uamuzi huo ambapo inadaiwa iwapo serikali itaamua kumchukulia hatua atakuwa tayari kuwataja vigogo wote waliokuwa wakiomba fedha ndani ya wakala huo.

Wakati huo huo, taarifa hizo zilifafanua kuwa kwa sasa ameandika barua akieleza kuwa amepata nafasi ya masomo nchini Uingereza kwa ajili ya shahada ya uzamivu ya ‘Civil Engineering’.

Uamuzi huo wa Mrema kuelekea nje ya nchi umeelezwa kuwa ni wa kutaka kukwepa ushahidi, kwa kile kilichoelezwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kuwa inaweza kumchunguza kwa tuhuma za kuisababishia hasara serikali.

Alichokosea Zitto Zuberi Kabwe ni Hichi


Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela aliandika kitabu chake cha kwanza akielezea maisha yake tangu akiwa wakili hadi alipotoka gerezani kiitwacho “A long walk to freedom”. Waliokisoma watakubaliana na hoja yangu ninayoijenga hapa.

Mandela anaeleza kwamba alipokuwa gerezani kisiwani Robin vuguvugu mle jela lilikuwa likiendelea na ilifika mahala wafungwa walikuwa wakikubaliana ni aina gani ya mgomo wataufanya.

Mara nyingi walikuwa wanaishia kugoma kula (hunger strike). Lakini Mandela anaeleza kuwa binafsi hakuwa anaipenda migomo ya kula. Hivyo kila lilipoletwa wazo la kugoma kula Mandela alikuwa kwenye upande wa waliopinga wazo lile na mara zote ilibidi wafikie muafaka kwa kupiga kura. Kwamba tugome kula au tusigome.

Mandela anaeleza kuwa siku zote wenye wazo la kugoma kula walishinda kwa wingi wa kura.  Endelea kusoma habari hii
                    

Alichokosea Zitto Zuberi Kabwe ni Hichi


Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela aliandika kitabu chake cha kwanza akielezea maisha yake tangu akiwa wakili hadi alipotoka gerezani kiitwacho “A long walk to freedom”. Waliokisoma watakubaliana na hoja yangu ninayoijenga hapa.

Mandela anaeleza kwamba alipokuwa gerezani kisiwani Robin vuguvugu mle jela lilikuwa likiendelea na ilifika mahala wafungwa walikuwa wakikubaliana ni aina gani ya mgomo wataufanya.

Mara nyingi walikuwa wanaishia kugoma kula (hunger strike). Lakini Mandela anaeleza kuwa binafsi hakuwa anaipenda migomo ya kula. Hivyo kila lilipoletwa wazo la kugoma kula Mandela alikuwa kwenye upande wa waliopinga wazo lile na mara zote ilibidi wafikie muafaka kwa kupiga kura. Kwamba tugome kula au tusigome.

Mandela anaeleza kuwa siku zote wenye wazo la kugoma kula walishinda kwa wingi wa kura.

Hadi hapa hakuna tofauti na CHADEMA kupiga kura kugomea hotuba ya Rais Kikwete yaani “Walkout”. Pia hakuna tofauti ya Zitto Kabwe na Mandela hadi hapa. Mandela hakupenda “hunger strike” wakati Zitto hakupenda “Walkout”. Kina Mandela walishindwa maoni yao kwa kura kama Zitto na wenzake walivyoshindwa juzijuzi.

Sasa tuone utekelezaje wa maamuzi ya upigaji kura kati ya Zitto Kabwe na Nelson Mandela.

Mandela anaeleza kwamba japo hakuunga mkono wazo la “hunger strike” lakini baada ya matokeo ya kura yeye ndiye aliyekuwa kinara wa kusimamia kugoma.
Na anaeleza kuwa kama msimamizi mgomo unapofika siku ya tatu alitegemea kuona ndoo za vinyeshi ziwe kavu lakini anashangaa kuona zikiwa na vinyesi vya hapa na pale kwa maana ya kwamba kuna watu walikuwa wanachomoka kimyakimya na kujificha na kwenda kula kwa kushindwa kuvuilia njaa.

Anaieleza hii kama kichekekesho lakini Mandela anaeleza jinsi ambavyo wagomaji walitakiwa kuonyesha umoja mara tu baada ya matokea ya kura. Kwamba hata kama bado kuna watu walitoroka kwenda kura lakini walifanya kwa siri sana na hadi anaandika kitabu hakuwajua.

Mandela anatufundisha nini? Anatufundisha kwamba haia haja ya kupiga kura kama wote mna wazo moja mnalotaka litumike. Ila kama kila mmoja ana wazo lake kinachofuta ni kujadiliana na kupima sababu na hasara za kila wazo.

Yakishindikana yote basi hamuwezi kupoteza muda mkijadiliana wakati uamuzi unatakiwa ufikiwe. Ndipo hapo mnaposema hoja zenu wote ni safi lakini kwa vile tumeshindwa kutoa uamuzi kwa njia ya ushawishi na maoni basi kura ndiyo iwe uamuzi utakaoheshimiwa.

Hata kwenye soka tena ya watoto wadogo tunaelewa kuwa inawezekana timu ikapenda kuanzia mechi kwenye goli la kusini labda kwa sababu siku hiyo upepo unawasaidia kutokea kusini. Kama timu pinzani haioni shinda kuanzia kaskazini basi hakuna sababu ya kupiga kura kwa kurusha shilingi.

Lakini kama wote Timu A na Timu B wanagombania golila kuanzia basi wanaweka rehani maamuzi yao kwenye matokeo ya kura. Kwamba watafuata matokeo ya kura ili kuamua cha kufanya yaani kuannzia wapi. Ndipo hapo kura inapigwa kwa kurusha shilingi. Hapa hakuna cha kur kulingana. Lazima shilingi itatoa maamuzi. Ama Timu A itashinda kwa kuanzia kusini ama Timu B.

Baada ya kupigwa kura kama walivyofanya kina Mandela au kurushwa shilingi zilivyofanya zile timu hakuna majadiliano mapya tena. Kugomea uamuzi wa kura ni sawa na kugomea maamuzi yaliyokubaliwa.

Ndiyo maana Mandela analifafanua hili kwamba japo yeye siku zote amepinga kwa hoja na kura kwamba hapendi hunger strike lakini pamoja na kushindwa amekuwa akiwa kinara wa kusimamia mgomo. Mandela anaonyesha nidhamu ya maamuzi. Alishindwa kupinga mgomo kwa ushawishi wa hoja, kisha akashindwa kwa kura hakuwa na jinsi kuukata uamuzi wa walio wengi.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Nelson Mandela, shujaa anayeheshimika duniani kote. Je, ndivyo ilivyokuwa kwa Zitto Kabwe? Wote tumejua sivyo.

Kwanza bila Zitto tusingejua maamuzi yale yalifikiwa vipi. Hivyo Zitto katusaidia kujua kuwa yalifikiwa kwa kupiga kura. Kumbe demokrasi waliyotumia kina Mandela mle gerezani ndiyo demokrasia waliyotumia CHADEMA.

Siungani na wanaolaumu Zitto kwa kutoa siri ya kilichofanyika kwani kwa katufunulia walipiga kura katuonyesha kwamba CHADEMA ni chama makini kinachoheshimu maoni ya watu na si kuendeshwa na udikteta.

Sasa baada ya kupiga kura ilitakiwa kufanya nini? Hapa Zitto anatofautiana na Mandela. Mwenzake Mandela aliamua kuwa kiongozi wa mgomo lakini Zitto hafanyi kama Mandela. Zitto alipiga kura lakini hafanyi kulingana na matokeo ya kura. Zitto anasahau kuwa kama kundi lake lingeshinda CHADEMA wangefanya kama alivyotaka yeye. Sijui napo angeenda BBC na kusema kuwa CHADEMA haikugoma kwa sababu waliokataa mgomo walikuwa wengi?

Mandela anawafundisha watu kama Zitto kwamba maamuzi yoyote yaheshimiwe maadamu hayajafikiwa kwa njia ya udikteta.

Zitto hata kama tunampenda vipi lakini mbele ya kadamnasi katuonyesha kuwa ana utovu wa nidhamu ya maamuzi. Kukataa maamuzi ni utovu wa nidhamu. Utovu ambao Mandela hautaka kuushiriki hata kama hakupenda la walio wengi.

Zitto angesema kwamba hakupiga kura kabisa, mimi nigekuwa wa kwanza kumuelewa na kumtetea. Hata mtoto wa darasa la tatu anajua nini cha kufanya baada ya matokeo ya kura. TUmecheza michezo mingi utotoni inayohusisha kupiga kura. Leo umepiga kura, wenzako wengi wamesema wanataka kugoma. Matokeo yanatoka badala ya kuyaheshimu wewe unafanya unavyotaka na unanung’unika. Hivi neno utovu wa nidhamu litumike kwa vitendo gani kama si hivi!

Kama CHADEMA au Zitto mwenyewe wana mpango wa kuuwajibisha utovu huu wa nidhamu basi huu ndiyo wakati muafaka ikiwa bado mapema na wengi wakiwa nalo kichwani. Ni kweli kunaweza kuwa na mgawanyiko lakini kazi ya kuelewesha itakuchukua muda na watu wataelewa polepole wale wasiotaka kuelewa mapema. Mkisubiri utovu huu muushughulikie zaidi ya 2012 au 2013 wakati uchaguzi wa 2015 umekaribia basi mgawanyiko unaweza kuingia hadi wakati wa uchaguzi na ikala kwenu.
Taarufa kwa hisani ya Global Publishers

Putin warns Russia will step up nuclear defense without new arms deal


In an interview with CNN host Larry King, Russian Prime Minister Vladimir Putin spoke of threats that might emerge if no agreement on missile defense in Europe and the New START treaty is reached.
Vladimir Putin said that if the US fails to seal the new deal, Russia will have no choice but to build up its nuclear forces.
Among other issues discussed on the primetime talk show were the diplomatic cable leaks released by WikiLeaks.
“Leaks such as this one have happened before, which is why I don’t see any catastrophe in this [situation],” Putin said.
However, the prime minister did speak with sharp criticism about the diplomats’ opinions of his relations with President Dmitry Medvedev.
“Frankly speaking, we did not suspect that [this assessment of Putin-Medvedev relationship] would be made with such conceit, crudeness and in such an unethical manner,” Putin said.
Putin's interview airs on CNN on Wednesday evening in the US.

Baada ya kutoa nyaraka za siri zaidi ya elfu kumi kuhusu Marekani, Interpool yatoa waranti ya kumkamata mmiliki wa Wikileaks


Mmiliki mtandao wa Wikileaks Julian Assange.Mmiliki mtandao wa Wikileaks Julian Assange.

Polisi ya kimataifa Interpol imemtaja Julian Assange mmiliki wa mtandao wa Wikileaks kuwa miongoni mwa watu wakuu inayowasaka. Waranti ya kukamtwa kwa Assange iliyotolewa na Interpol ina maana kwamba huenda Assange akakamatwa kokote. Hapo awali mmiliki huyo wa Wikileaks alikata rufaa dhidi ya amri ya kukamtwa kwake iliyotolewa na Sweden kwa kumtuhumu kwa ubakaji.

Ukurasa katika mtandao wa Wikileaks.Ukurasa katika mtandao wa Wikileaks.















                                                   Endelea kusoma habari hii

Membe: Tunaiunga mkono Palestina

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema Tanzania itaendelea kuwaunga mkono watu wa Palestina katika jitihada za kutafuta uhuru wa taifa lao kutoka kwenye mgogoro wa kisiasa kati yao na Israel.
Waziri Membe aliyasema hayo jana katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na wananchi wa Palestina, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Akitoa hotuba katika maadhimisho hayo, Waziri Membe alisisitiza kile alichokiita msimamo wa siku nyingi wa Tanzania juu ya mgogoro huo wa Mashariki ya Kati, ambao ni kutaka kuwapo kwa mataifa mawili huru likiwamo la Palestina huru itakayoishi katika mazingira ya amani na usalama na Israel.

“Tutaendelea kuusimamia msimamo wetu wa tangu mwaka 1961 na kushirikiana na watu wa Palestina katika jitihada za kutafuta uhuru wao kwa njia ya amani,” alisema Waziri Membe.

Mara kwa mara serikali imekuwa ikiurejea msimamo huo wa kidiplomasia inapotoa rai yake kwa jumuiya za kimataifa likiwemo taifa la Marekani katika kumaliza uhasama wa mataifa hayo mawili.

Mwanzoni mwa mwezi uliopita serikali kupitia kwa balozi wake katika Umoja wa Mataifa, Ombeni Sefue, ilipongeza juhudi zinazofanywa na serikali ya Marekani za kuanzisha tena mazungumzo ya kutafuta amani kati ya Israel na Palestina.

“Tanzania pia inaunga mkono suala la kuwapo kwa mataifa mawili huru likiwamo la Palestine huru wakiishi sambamba katika mazingira ya amani na salama na taifa la Israel huku tukiunga mkono haki ya Waisrael kuishi kwa amani,” alisema Balozi Sefue mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipokuwa likijadili taarifa ya Kamati Maalum iliyohusika na uchunguzaji wa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wananchi wa Palestina unaofanywa na Israel, mwanzoni mwa mwezi Novemba, mwaka huu.

Kwa upande wake, Balozi wa Palestina nchini, Dk. Nasri Khalil Abu Jaish, aliishukuru Tanzania kwa kuendelea kuiunga mkono na kuisaidia Palestina katika jitihada za kuufikia uhuru kamili wa taifa hilo.

Aidha, balozi Abu Jaish alizitaka Jumuiya za Kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa kuingilia kati mgogoro wa Mashariki ya Kati na kuhakikisha watu wa Palestina wanapewa ardhi na uhuru wao unaodhibitiwa na Israel.

JK awapa maumivu Makamba, Malecela

UTEUZI wa Rais Jakaya Kikwete wa Mawaziri na Manaibu wake, umeacha maumivu kwa familia za wakongwe wa siasa nchini, Mzee John Samuel Malecela na kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, Tanzania Daima Jumatano, limebaini.
Duru za siasa kutoka ndani ya chama hicho tawala zinasema kuwa wakati familia ya Malecela aliyepata kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, ikiumizwa kwa Anne Kilango Malecela kuachwa kwenye baraza hilo, familia ya Makamba nayo imepata maumivu hayo baada ya mtoto wao, Januari Makamba aliyetazamiwa kupewa uwaziri, kuachwa nje.

Vyanzo vyetu vya habari vililiambia Tanzania Daima Jumatano kuwa Januari Makamba tangu alipotangaza nia ya kuwania jimbo la Bumbuli na kupita bila kupingwa, amekuwa akitajwa na watu wengi nje na ndani ya CCM kwamba angeweza kuteuliwa kuwa Waziri au Naibu wa wizara yoyote.

Sababu zilizokuwa zikimpa Januari nafasi ya kuteuliwa kushika uwaziri ni pamoja na kudaiwa kuwa kijana mwenye elimu nzuri huku sifa hiyo ikiwa imetamkwa mara kadhaa na Rais Kikwete mwenyewe.

Sanjari na kuwahi kummwagia sifa kijana huyo, Rais Kikwete pia kwa upande mwingine aliwahi kuahidi huko nyuma kwamba baraza lake lijalo lingekuwa la vijana zaidi.

Sababu nyingine ni Januari kuwa karibu na Rais Kikwete akifanya naye kazi Ikulu kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kama msaidizi wake wa karibu, huku uswahiba wa baba yake, Mzee Makamba, na mkuu huyo wa nchi pia ukipewa nafasi.

“Januari mwenyewe alijua angeteuliwa, Mzee Makamba alijiridhisha kabisa kwamba mwanaye angekuwemo kwenye Baraza, lakini uteuzi uliofanywa na Rais umemuumiza sana Mzee Makamba na hadi sasa haamini kilichotokea,” alisema mmoja wa wana CCM kutoka ofisi ndogo ya Lumumba, jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, wadau wa siasa kutoka ndani na nje ya CCM bado wanampa nafasi kubwa Januari kuteuliwa kwenye moja ya wizara zisizo na manaibu kwa sasa au wakati wowote Rais atakapoamua kufanya mabadiliko madogo au makubwa.

Wakati familia ya Makamba ikiuguza maumivu hayo, familia nyingine ya mkongwe wa siasa nchini, Malecela, nayo imeachwa na maumivu kutokana na Anne Kilango pia kuachwa nje ya uteuzi.

Mama Kilango, mmoja wa wanasiasa waliojipatia sifa katika Bunge la tisa lililopita kutokana na ujasiri wake wa kuwalipua mafisadi hadi kutunukiwa Tuzo ya Martin Luther King, amekuwa akitajwa na duru za siasa kwamba angekuwemo ndani ya baraza jipya.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata, zinadai kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu, Mama Kilango alipata kuahidiwa kuwa Waziri, lakini aliambiwa aongeze elimu na mwaka jana alitunukiwa shahada yake ya kwanza ili kujiweka sawa kwa uongozi huo.

“Mama Kilango amesoma, amepata digrii yake ya kwanza, anajiandaa kuingia tena darasani apate digrii ya pili na hii yote ni kutokana na kuahidiwa uwaziri, lakini alipewa sharti aongeze elimu,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Sababu nyingine inayotajwa kumpa maumivu Malecela ni ukweli kwamba yuko nje ya Bunge na hana nafasi yoyote muhimu kwenye chama, ukiachilia ile ya kuwa mjumbe wa kudumu wa Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu wa CCM.

“Malecela kwa sasa si Mbunge na alipoangushwa kwenye kura za maoni, alilalamika ndani ya chama akitarajia huruma ya Rais, lakini aliachwa, hivyo uteuzi wa Mama Kilango kuwa Waziri, ungempa faraja kubwa,” alisema mtoa habari wetu.