AIBU BOSI WA BANDARI AFUMWA AKILA URODA

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Na Mwandishi Wetu
Ofisa Mwandamizi Uchukuzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Makao Makuu jijini Dar, Kitengo cha Makontena, Peter Milanzi (54) amejikuta ndani ya aibu nzito kufuatia madai kwamba, amekutwa akiwa na mke wa mtu kwenye nyumba ya kulala wageni ‘gesti hausi’, Ijumaa Wikienda linashuka na ‘diteilzi’. 

Tukio hilo lililoacha historia, lilijiri Desemba Mosi, 2010 (Siku ya Ukimwi Duniani) majira ya alasiri kwenye chumba namba tano cha hoteli moja (jina tunalo), Buguruni, Dar.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mume aliyejitambulisha kwa jina la Shaha Juma alidai kumbamba Milanzi akiwa na mkewe wa ndoa aitwaye Salia.

Chanzo hicho kikaongeza kudai kuwa, kabla ya fumanizi hilo lililokusanya mashuhuda kibao, mume wa mwanamke huyo alikuwa na kibarua kizito cha kufuatilia nyendo za ‘wezi’ hao mpaka ndani ya chumba hicho.
“Unajua jamaa kabla hajawabamba, alifuatilia kwa karibu mno nyendo zao za siku hiyo mpaka wanaingia hapa gesti, pia akahakikisha anakijua na chumba,” kilisema chanzo hicho. 

Chanzo hicho kiliendelea kuanika kweupe kwamba, baada ya mwanaume huyo kujiridhisha kwamba, mkewe Salia na mzee huyo wamo ndani ya chumba hicho, aliita mashahidi ambao hawakutajwa majina ili kushuhudia tukio hilo.

Inadaiwa kuwa, mlango uligongwa na mume wa mwanamke huyo alizama ndani sanjari na mashahidi wake na kuanza kumhoji Bw. Milanzi kisa cha kuingia gesti na mke wa mtu ambapo alibabaika katika utetezi.

Lakini kwa upande wa pili, habari zilizopatikana kutoka kwa wahudumu wa gesti hiyo zinadai kwamba, Milanzi alijitetea kwa kusema kuwa, kama ni lawama basi mwanamke huyo ndiye anayetakiwa kubebeshwa, kwani hakuwahi kumwambia mzee huyo kuwa yeye ni mke wa mtu.

Aidha, ilisemekana kuwa, mbali na mwanamke huyo kutosema ni mke wa mtu, lakini pia hakuwa na dalili zozote zinazoonesha kuwa ameolewa, kama vile pete au hofu ya muda.
Ijumaa Wikienda lilimsaka Shaha na kumuuliza kama kuna ukweli wa madai hayo ambapo alikiri.

“Ni kweli, mke wangu nimemkuta chumba cha gesti na mwanaume, lakini nimeshawahi kumuonya kwa simu mara kadhaa huyu mzee aache kumchukua mke wangu, hakutaka kusikia,” alisema mume huyo.

Akaongeza: “Taarifa za tukio zipo Buguruni Polisi lakini RB ipo nyumbani (hakusema ni wapi) na kwa wakati huu siwezi kurudi kwa sababu nipo kazini.”

Wikienda lilipofika Kituo cha Polisi Buguruni, lilikosa ushirikiano kutoka kwa askari waliokuwa zamu siku ya Ijumaa baada ya kudai kuwa wao si wasemaji wa jeshi hilo.

Kwa upande wake, mzee Milanzi alipopatikana kwa simu yake ya mkononi siku ya Ijumaa alikiri kutokewa na tukio hilo, lakini akasema ‘amechoreshewa’.
“Ni kweli mkasa umenikuta, lakini umechezeshwa tu na watu. Yule mwanamke hajasema ameolewa,” alisema.

Mzee huyo aliongeza kuwa alipenda kufika kwenye ofisi za gazeti hili, Bamaga- Mwenge ili kuweka wazi kila kitu lakini akasema kwa bahati mbaya alikuwa safarini Morogoro. 

Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, dakika chache baada ya ‘mtuhumiwa’ huyo kumaliza kuongea utetezi wake, simu yake iliingia kwa mwandishi wetu ambapo sauti ya mtu mwingine ilisikika ikivurumisha matusi huku ikidai kama habari hii itatoka gazetini watu wataoneshana kazi mjini.

“Ninyi ni matepeli tu, hamna lolote, mnaunganisha unganisha picha halafu mnawasingizia watu, ala…(tusi), nakwambia hivi, ninyi…(tusi) kama hii habari itatoka basi hapa mjini (Dar) tutaoneshana kazi, si mnajifanya watoto wa mjini,” ilisema sauti hiyo na kukata simu.

Baada ya dakika tano, simu ya Milanzi iliingia tena kwa mwandishi na alipoipokea, sauti ya Milanzi ilisikika ikisema:

“Unajua bwana haya mambo yana utata mkubwa, mimi nimeonewa, hapa nilipo imebidi niwasiliane na watu wa Ikulu ili kuona tunafanyaje.”

Mwandishi wetu alimpa ‘kibali’ mzee huyo cha kuendelea kuwasiliana na watu wa Ikulu kama alivyodai lakini alimpa angalizo kuhusu watu wanaotumia simu yake kutukana na kukejeli.

0 comments: