NAPE ALIVYOWASHA MOTO MBEYA

Wabunge wa  CCM wa mkoa wa Mbeya na kwengineko wakimuongoza Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauyem kuingia uwanja wa Rwandanzovwe mjini Mbeya kwenye mkutano mkubwa wa hadhara Katibu wa Vijana na Jimbo la Mbozi wa Chadema Warren Kaminyonga akionyesha kadi yake ya CHADEMA kabla ya kumkabidhi NAPE
 Nape akimkaribisha  Mwenyekiti wa Mtandao wa Chadema wa wanataaluma Prince  Mwaihoja
 Nape akihutubia maelfu ya watu katika uwanja wa Rwandanzovye mjini Mbeya
 Mh. Samwel Sitta akihutubia katika mkutano huo
 Nape akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Rwandanzovwe mjini Mbeya 
 Mjumbe wa NEC, Oganaizesheni Asha Abdallah Juma akihutubia
 Mbunge wa Simanjiro Mh.  Ole Sendeka akihutubia
 Mwenyekiti wa Wabunge wa mkoa wa Mbeya, Prof Mwakyusa akizungumza. Kushoto ni Nape
 Maelefu ya watu  kwenye uwanja wa Rwandanzovwe mjini Mbeya
 Mbunge wa Kyela Dkt. Harrison Mwakyembe akihutubia kwenye mkutano huo
 Nape akicharaza gita wakati wa mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Rwanda, Nzovwe, mjini Mbeya
 Wabunge wa mkoa wa Mbeya, Sitta na Nyarandu wakimuongoza Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kuingia uwanja wa Rwandanzovwe mjini Mbeya kwenye mkutano wa hadhara
Msafara wa pikipiki ukipokea msafara

Zitto akalia kuti kavu • DK. SLAA ASHANGAZWA NA TAARIFA

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, hivi sasa yuko katika wakati mgumu na huenda akavuliwa wadhifa wa Unaibu Katibu Mkuu.

Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa kikao cha Kamati Kuu ambayo kilianza jana na kumalizika leo kinaweza kufikia uamuzi huo baada ya wabunge wa chama hicho juzi kuamua kumvua Zitto wadhifa wa Naibu Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni. Endelea Kusoma Habari Hii...

Dk. Slaa aanza mashambulizi • ASEMA MAFISADI WASUBIRI KIAMA CHAO

KATIBU mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbrod Slaa, amesema kuwapo kwake nje ya Bunge hakumfanyi aache kupambana na mafisadi na vitendo vya kifisadi.

Dk. Slaa, alisema mafisadi ... Endelea Kusoma habari hii..

JK Atunukiwa tena Shahada ya Heshima

Image
Rais Jakaya Kikwete akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Afya ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na Mkuu wa chuo hicho, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) wakati wa Mahafali ya nne ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi, Dk Shukuru Kawambwa (kulia) na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Deogratius Ntukamazina. 

Zitto adai amelishwa sumu

Image
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Kabwe Zitto, akipatiwa kipimo na Muuguzi, Flora John,wa Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam ambako amelazwa baada ya afya kuzorota ghafla. 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye jana aliruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam alikolazwa kwa matibabu ya tumbo amedai kuwa matatizo hayo aliyapata baada ya kula chakula chenye sumu.“Namshukuru Mungu naendelea vizuri na nimesharuhusiwa kutoka hospitali, Endelea Kusoma habari hii...

Wasanii hawa kuandaa Movie Kuhusu Mmiliki wa WikiLeaks Julian Assange??

                                                   Brad Pitt with Angelina Jolie


American filmmaker Michael Moore intends to do a biopic about WikiLeaks founder Julian Assange, reports American movie website The Wrap.
Moore has posted positive comments about WikiLeaks and Assange in his blog and Twitter account.
But Moore could already be too late as there are another three serious projects in Hollywood about Assange, and for one of them the reported budget is $100 million. Another could get some $50 million in financing and is said to have David Fincher working on it with Brad Pitt rumored to play Julian Assange. (click here to see what is in WikiLeaks website)
                                                                     David Fincher


                                                               Michael Moore


                        Julian Assange, Mmiliki wa WikiLeaks aliyekamatwa hivi karibuni

CHADEMA wapiga kura ya kutokuwa na Imani na Zitto Kabwe

Image
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Kabwe Zitto, akipatiwa kipimo na Muuguzi, Flora John,wa Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam ambako amelazwa baada ya afya kuzorota ghafla. 
KAMA ilivyotarajiwa na wengi, mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe amevuliwa wadhifa wake wa unaibu kiongozi wa upinzani bungeni, lakini chama hicho 'kikapigwa jeki' baada ya mfanyabiashara maarufu, Mustafa Sabodo kukipa Sh150 milioni kwa ajili ya kujenga chuo cha maadili ya uongozi.

Matukio hayo mawili pia yaliambatana na kuugua ghafla kwa Zitto na makamu mwenyekiti wa Chadema, Said Amur Arfi ambao wamelazwa Hospitali ya Aga Khan kwa matatizo tofauti... Soma habari Kamili

Vigogo kutinga mahakamani kesi za uchaguzi

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), imesema wakati wowote kuanzia sasa itakamilisha uchunguzi na kuwafikisha mahakamani vigogo wa serikali wanaokabiliwa na tuhuma za rushwa katika uchaguzi mkuu uliopita. Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah, alibainisha hayo jijini Dar es Salaam jana, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Katika maadhimiho hayo, Dk Hoseah alisema iwapo viongozi walio madarakani watabainika kujihusisha na rushwa katika mchakato huo, watapandisha kizimbani na sheria itachukua mkondo wake.

“Bado tupo kwenye mapambano, mpaka sasa mchakato wa upelelezi wa kesi hizo unaendelea, mara tu utakapokamilika kesi hizo zitaanza kufikishwa mahakamani, ” alisema Dk Hoseah na kuongeza: Nchi hii inaendeshwa kwa utawala wa sheria, huwezi kumpeleka mtu mahakamani bila kuwa na ushahidi, tukiwa tunakimbilia mahakamani nchi hii tutaiporomosha.” Pia, Dk Hosea alisema rushwa ni jambo linalohitaji kufanyiwa kazi kwa muda mrefu ili kufanikisha kutokomezwa, lazima mapambano yake yahusishe kila mwananchi.

Dk Hosea alisema kuhakikisha wanafanikiwa kwenye vita hiyo hasa kwa taasisi za umma, wameanzisha kamati 200 katika wizara na idara mbalimbali za serikali. Alisema wameanzisha kamati 123 katika halmashauri mbalimbali nchini, aliwataka wananchi kutumia kamati hizo kuweza kupambana na rushwa.

Waakati Takukuru ikieleza hayo, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limeitaka serikali kukamilisha mchakato wa kupitisha sheria ya kulinda wananchi watakaojitokeza kufichua vitendo vya rushwa. Mwakilishi wa UNDP nchini, Philippe Poinsot, alisema serikali inatakiwa kukamilisha mchakato wake wa kupitisha sheria ya kulinda wananchi watakaoshiriki kufichua wanaotoa na kupokea rushwa.

Poinsot alisema serikali inatakiwa kuwa wazi katika masuala ya ununuzi bidhaa na huduma zake na kwamba, suala hilo linachukua asilimia 70 ya bajeti ya serikali. Mwisho

Asasi zataka Katiba mpya

MTANDAO huru wa asasi za kiraia zilizojikita kufanya uangalizi wa Uchaguzi Mkuu Mkuu 2010 (TACCEO), umetoa ripoti kuhusu uchaguzi huo huku ukipendekeza mabadiliko ya katiba na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.
Wakati waangalizi hao wakitoa ripoti hiyo yenye kurasa 300 ambayo imeeleza kwa kirefu upungufu uliojitokeza na kupendekeza mabadiliko ya katiba, serikali ya Kenya imesema jukumu la kudai Katiba ni la wananchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Balozi wa Kenya nchini, Mutinda Mutiso, alipokuwa akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya haki za binadamu dunia yaliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na na Haki za Bindamu (LHCR) na kuadhimishwa jjijini Dar es Salaam jana.

Mutiso alisema ingawa Kenya ilichukua muda wa miaka 20 kupata katiba mpya, Tanznaia kazi hiyo inawezekana na muda huo unaweza kupungua kwa kutumia uzoefu toka Kenya
“Sisi tunamshukuru Mungu tumepata Katiba mpya mchakato wa ni mgumu na huchukua muda mrefu, lakini hilo kwa hapa linawezekana tena muda unaweza kupungua,” alisema Mutiso.

Mutiso alipongeza Watanzania kwa kufanya uchaguzi na kumaliza kazi hiyo kwa amani na utulivu na kuomba, hali hiyo iendelee kuenziwa.
Kwa upenda wake, Mwenyekiti wa (Tacceo), Martina Kabisama, alisema kasoro nyingi zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu, zilitokana na upungufu uliopo kwenye Katiba na Tume ya uchauzi.

“Tumefanya kazi ya uangalizi wa uchaguzi nchi nzima, tusema bila wago kuwa katika baadhi ya maeneo watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi waliegemea chama tawala na kusahau majukumu yao,” alisema Kabisama na kuongeza:
“Wapo waliochelewa kutangaza matokea makusudi kwa lengo la kuchezea haki za watu na hata kusababisha vurugu maeneo hayo, hiyo ilitokana na matokeo ya watendaji wa tume kuwa waajiriwa na wakati mwingine kuwajibika kwa aliowateua.”
Kabisama alisema inatakiwa kuundwa Tume huru ya uchaguzi itakaoyoajiri wafanya kazi wake kila majimbo na kwamba, watu hao watashughuka na uchaguzi pekee.
Naye Salumu Bar’wan, Mbunge wa Lindi Mjini kupitia CUF, alisema watu wanaopinga mabadiliko ya katiba wana masilahi binafsi.

Bar’wan alisema katiba hiyo ina upungufu mkubwa ambao kimsingi inatakiwa kuandikwa upya.
Naye Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Sengondo Mvungi, alisema kazi iliyopo hivi sasa ni kwa wanaharakati na wapenda mabadiliko kutoa elimu kwa Watanznaia juu ya umuhimu wa katiba mpya.
Dk Mvungi alisema kama Watanznaia wataelewa maana ya katiba na umuhimu wake, watashiriki kikamilifa kuidai.

KILIMANJARO STARS YATINGA FAINALI KWA KUIFUNGA UGANDA BAO 5-4 KWA MATUTAWachezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars wakishangilia ushindi walioupata dhidi ya Ugannda 'The Craners' kwa mikwaju ya penati 5-4 na kupata tiketi ya kuingia fainali ya mashindano ya Tusker Challange Cup katika mchezo uliopiga jioni ya leo ndani ya Uwanja wa Taifa,jijini Dar. kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars itamenyana na Ivory Coast katika fainali ya mashindano ya Tusker Challange Cup hapo jumapili ya Desemba 12.


Balozi Mbita ataka mabadiliko ya Katiba


BALOZI Hashim Mbita ambaye alikuwa Katibu wa Kamati ya Ukombozi ya uliyokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) amewashangaa wanasiasa wanaoogopa kuifanyia mabadiliko katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza katika Televisheni ya Taifa jana asubuhi, Balozi Mbita alisema: “Katiba yetu ina ukakasi, hivyo inahitaji kufanyiwa mabadiliko ili iweze kwenda na wakati na mfumo wa kisiasa ulipo sasa na kudumisha umoja wa kitaifa”.

Alifafanua kuwa katiba iliyopo inaweka sera za maendeleo mikononi mwa wahisani ambao huamua hatima ya nchi, hivyo kuzorotesha juhudi za maendeleo.

Balozi Mbita alitoa mfano kuwa wafadhili walishawahi kukataa utekelezaji wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria mpaka mkoani Shinyanga kwa kuwa haukuwa katika vipaumbele vyao.

Kauli hiyo ya Mbita inakuja wakati kumeibuka mjadala mkali katika jamii kwa wanaharakati na vyama vya upinzani vitaka mabadiliko ya katiba huku viongozi wa chama tawala wakiwemo wabunge na mawaziri wakipinga hatua hiyo.
Hivi karibuni, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Celina Kombani alisema katiba haiwezi kubadilishwa na kwamba hajui madai ya wapinzani kuhusu yanahusu nini na kwamba hawezi kushghulikia kwa vile hajapelekewa rasmi maelezo ya mambi yanayotakiwa kubadilishwa.

Wabunge wa Chadema walisimama na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kusima ili kutoa hotuba ya kufunga rasmi Bunge la kumi la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania wakidai kuwa hawakubaliani na katiba iliyomweka madarakani kwa kuwa ina kasoro nyingi.

Kitendo hicho kiliamsha changamoto mpya katika jamii ya Watanzania wakiwemo vijana na wasomi ambao wanasema sasa umefika wakati wa kuifanyia mabadiliko Katiba kwa manufaa ustawi taifa.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Gaudence Mpangala, ambaye alishiriki katika kipindi hicho cha TBC alisema katiba mpya italinufaisha taifa kwa kuboresha misingi ya uongozi bora na siasa safi nchini kwa sababa iliyopo sasa haiendi na wakati, mfumo wa siasa na sera za taifa.

Barack Omama faces heavy critcs


Obama won’t get renominated if tax deal goes through

UN: Ouattara ndiye mshindi Ivory Coast

Wananchi wa Ivory Coast wakizungumzia mzozo wa kisiasa nchini mwao. Jamii ya kimataifa yasema kiongozi wa upinzani Alassane Ouattara ndiye aliyeshinda na wala sio Rais wa sasa Laurent Gbagbo
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limetoa taarifa inayomwidhinisha kiongozi wa upinzani nchini Ivory Coast, Alassane Ouattara kuwa ndiye aliyeshinda kura ya urais -- na wala sio rais wa sasa, Laurent Gbagbo, ambaye amejaribu kujitangaza mwenyewe kuwa mshindi.

Awali Urusi ilikuwa imeelezea wasiwasi kwamba kwa kumtangaza bwana Ouattara mshindi, umoja wa mataifa utakuwa umezidisha majukumu yake.
Uamuzi wa baraza hilo uliokumbwa na pingamizi kutoka kwa Urusi sasa umeimarisha shutuma za kimataifa dhidi ya rais Laurent Gbagbo, ambaye ameendelea kupuuza wito wa jamii ya kimataifa wa kumtaka ajiondoe madarakani.
Jana Jumatano, afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast, Choi Young-jin, amesema tathmini yake ya matokeo ya uchaguzi imemshawishi kwamba wapiga kura walimchagua bwana Ouattara kama rai bila pingamizi yoyote.
Awali serikali ya bwana Gbagbo ilpuuzilia mbali wito kutoka kwa jumuiya ya kiuchumi kwa mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS, wa kumtaka ajiondoe madarakani.
Juhudi za umoja wa Afrika, AU za kujaribu kutatua mgogoro huo kupitia rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki hazijaonekana kupata mafanikio ya haraka.

Dkt Robert Ouko 'aliuwawa ikulu

Bunge la Kenya. Ripoti ya mauaji ya Dkt. Ouko ilitayarishwa miaka mitano iliyopita na kuwasilishwa bungeni jana Jumatano.
Ripoti iliyotarishwa na kamati ya bunge la Kenya miaka mitano iliyopita imedai kuwa aliyekuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni aliyekuwa na ushawishi mkubwa Robert Ouko, aliuwawa katika ikulu ya rais mjini Nakuru.
Ripoti hiyo iliyotayarishwa na kundi la wabunge wa Kenya inadai kuwa Bwana Ouko aliuwawa baada ya kutofautiana na waziri mwenzake katika serikali ya rais mustaafu Daniel Arap Moi wakiwa ziarani nchini Marekani.
Ripoti hiyo iliwasilishwa katika bunge la Kenya siku ya Jumatano. Ripoti hiyo inapendekeza kuchunguzwa kwa watu mashuhuri waliohudumu katika serikali ya rais mustaafu Daniel Arap Moi, wanaodaiwa kuhusika katika mauaji ya bwana Ouko.
Rais Mustaafu wa Kenya Daniel Arap Moi. Dkt. Robert Ouko aliuwawa wakati wa utawala wake.
Kadhalika ripoti hiyo inadai kuwa Bwana Ouko aliyeuwawa mwaka 1990, alikuwa tayari amefutwa kazi na walinzi wake kuondolewa juma moja kabla ya kutoweka kwake.
Ripoti hiyo inadai kuwa ubishi uliibuka kati ya Bwana. Ouko na waziri mwenzake baada ya waziri huyo kumkejeli kwa kumwita Ouko ''Bwana Rais''.
Mauaji ya Bwana Ouko yalizua tetesi kali nchini Kenya na ni mojawepo tu ya mauaji mengi ya kisiasa yanayodaiwa kutekelezwa na serikali ya Kenya tangu taifa hilo lijinyakulie uhuru mwaka 1963.
Uchunguzi wa kina wa mauaji hayo bado haujakamilika huku mfumo wa sheria nchini humo ukilaumiwa kwa kuwa kizingiti cha kupatikana ukweli.

Wahitimu kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afya wakila kiapo

Image
Wahitimu wa shahada ya Upasuaji na Dawa(MBBS) kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afya, IMTU wakila kiapo wakati wa mahafali ya nne ya Chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam

Udini ni ulaji wa wakubwa – Warioba


WAZIRI Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba amesema udini unaotajwa kuwapo nchini, hasa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, umo miongoni mwa viongozi si wananchi wa kawaida.
Kauli hiyo ya Jaji Warioba ni sehemu ya maoni yake ya maadhimisho ya miaka 49 ya Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika, Desemba 9, mwaka 1961 yanayofanyika kesho Alhamisi.

Amesema licha ya viongozi waasisi kufanikiwa kujenga Taifa moja, dalili za sasa si njema na kwamba kasi ya viongozi kugawanyika hata katika vyama vyao vya siasa inaelekea kutishia umoja wa nchi.

Katika mahojiano maalumu na Raia Mwema yaliyochapishwa katika kurasa za tisa na 10 za toleo hili, Jaji Warioba anasema wananchi kawaida wamekuwa wakiendelea na shughuli zao bila kuulizana dini wala kabila zao.

“Wanafanya shughuli zao za kawaida iwe za biashara au uzalishaji. Ukikuta kundi la Wamachinga utawakuta vijana wa kutoka sehemu mbali mbali, dini mbali mbali na kabila mbali mbali wanafanya shughuli moja, hawajibagui hata kidogo.

“Inapofika wakati wa uchaguzi ndipo unasikia haya mambo ya ukabila, ukanda na udini. Haya yanaletwa na hawa ambao wanatafuta madaraka. Hawa wanaotafuta madaraka ndio wameleta matumizi ya fedha katika kutafuta uongozi,” alisema Jaji Warioba.

Katika hatua nyingine, Jaji Warioba ambaye amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere, ameonyesha kukerwa na tabia mpya ya kutojiamini kama nchi kiasi cha kutegemea zaidi wafadhili.

“Kwa nini waasisi wetu walijiamini zaidi kuliko sasa hivi? Mimi nadhani wakati ule TANU inadai Uhuru tukiwa vijana ndiyo tumeingia kwenye siasa, hali ilikuwa ngumu sana. Endelea Kusoma Habari Hii..

Mawaziri Hawa Wanajaribu Kuipa Nchi Hadhi Yake

Kitendo cha baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya JK ambao wametoa kauli za utendaji mara baada ya kuapishwa zimechukuliwa na wananchi kama ni kitanzi kwao endapo maelekezo yao hayatakamilika, Risasi Mchanganyiko linashuka kikamilifu.

Mawaziri ambao wapo katika subira ya wananchi kufuatia kauli zao ni wale ambao wameshaongea na vyombo mbalimbali vya habari na kudos maonyo au maelekezo kuhusu wajibu wa wizara walizoteuliwa kuzitendea kazi.

Waziri John Magufuli.

Jumuiya ya ECOWAS yamtambua Ouattara kama rais wa Cote d´Ivoire

Alassane Ouattara atambuliwa na jumuiya ya ECOWAS kama rais mpya wa Cote d´Ivoire

Alassane Ouattara atambuliwa na jumuiya ya ECOWAS kama rais mpya wa Cote d´Ivoire
Viongozi wa nchi na serikali za Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika magharibi ECOWAS wamemtambua Alassane Ouattara kama Rais aliyechaguliwa nchini Cote d'Ivoire na kumtaka rais Laurent Gbagbo kukubali kushindwa

Baada ya mkutano wa dharura uliohudhuriwa na viongozi wa mataifa ya kanda hiyo, uliofanyika Abuja Nigeria, Jumuiya hiyo ya ECOWAS imemuongezea mbinyo zaidi Bwana Gbagbo kwa kuisimamisha nchi hiyo kujihusisha na kundi hilo.

Aidha, Rais wa muda wa ECOWAS, Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameonya dhidi ya juhudi za kuzuia makubaliano hayo, kama ilivyotokea nchini Kenya na Zimbabwe.

Awali Bwana Gbagbo alikataa kutekeleza matakwa ya kimataifa, ya kumtaka kukubali kushindwa na badala yake kutangaza baraza lake la mawaziri, ikiwa ni siku mbili tu baada ya mpinzani wake Alassane Ouattara kutangaza pia serikali yake, chini ya ulinzi wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa. Jana Gbagbo alifanya kikao cha kwanza cha baraza lake la mawaziri.

Mabishano yaliyozuka kufuatia matokeo ya uchaguzi wa rais nchini humo mwezi uliopita katika nchi hiyo iliyo maarufu kwa zao la kakao, yamezidisha hatari ya kutokea tena ghasia katika taifa hilo ambalo bado limegawanyika baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2002 na 2003, hali iliyosababisha pia Umoja wa Mataifa kuondoa baadhi ya wafanyakazi wake.

Kwa mujibu wa shirika la Kimataifa la Msalaba mwekundu, mapigano kati ya majeshi ya ulinzi na kati ya wafuasi wanaopingana wa viongozi hao yamesababisha vifo vya watu 28 na wengine 280 kujeruhiwa tangu Novemba 26.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan RiceBalozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice

Wakati huo huo, Katika Umoja wa mataifa wanadiplomasia wanasema kuwa Urusi imeipinga taarifa iliyotolewa ya kumtambua Alassane Ouattara kama Rais wa Cote d'Ivoire.

Wanadiplomasia wamearifu kuwa baada ya mazungumzo ya faragha yaliyodumu kwa takriban saa tano na nusu, mazungumzo hayo yaliahirishwa kwa siku kwa wajumbe wa Urusi kusema kwamba wanahitaji maelekezo zaidi kutoka Moscow.

Nafasi ya Urusi ni nguzo kubwa kwa sababu taarifa za Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa lazima ipitishwe na wote bila ya kupingwa, ikiwa na maana kuwa mwanachama yeyote akipinga maamuzi yaliyofikiwa atazuia hatua hiyo.


Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa,Susan Rice, ambaye kwa sasa ndiye rais wa mwezi wa baraza hilo amesema ana matumaini kuwa mjadala huo utaendelea leo.

Kwa upande wake, mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Afrika magharibi Y J Chio amethibitisha kuwa Ouattara ndiye mshindi, ambapo alilifahamisha baraza la usalama pia kwamba matokeo ya uchaguzi yalikuwa wazi na kwamba kulikuwa na mshindi mmoja tu.

Awali akithibitisha hilo alisema, '' Matokeo yamethibitisha tena Bwana Ouattara kuwa ni mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa Rais wa Cote d'Ivoire.''

Kuidhinishwa huko kwa Bwana Ouattara na Umoja wa mataifa kumemfanya Bwana Gbagbo kuwa na wafuasi wachache kimataifa baada ya jumuia ya ECOWAS pia kumtambua Ouattara

Sitta: Kuilipa Downs ni kuhujumu uchumi

ASEMA HIZO NI NJAMA ZA GENGE LINALOTAFUTA FEDHA ZA UCHAGUZI MKUU 2015
WAZIRI mpya wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri, amesema hatua yoyote ya kulipa fidia ya Sh 185 bilioni kwa kampuni ya Dowans, ni kuhujumu uchumi wa nchi.

Sitta, ambaye aliongoza Bunge la Tisa lililotikisa nchi kwa kuibua kashfa za ufisadi, pia amesema kuna kila dalili za genge linalohujumu nchi kuandaa mpango wa kutafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.

Sitta alikuwa akitoa maoni yake baada ya kuulizwa na Mwananchi kuhusu hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuhishi wa Kibiashara (ICC) iliyolitaka Shirika la Umeme (Tanesco) kuilipa Dowans Sh185 bilioni kutokana na kuvunja mkataba bila ya kufuata taratibu.

Tanesco ilivunja mkataba huo wa kuzalisha umeme mwaka 2008, ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya kuisha, ikieleza kuwa mkataba huo ulikiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma. Tanesco imesema itazungumzia suala hilo baada ya hukumu hiyo kusajiliwa nchini.

Mawaziri Hawa Wanajaribu Kuipa Nchi Hadhi Yake

Kitendo cha baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya JK ambao wametoa kauli za utendaji mara baada ya kuapishwa zimechukuliwa na wananchi kama ni kitanzi kwao endapo maelekezo yao hayatakamilika, Risasi Mchanganyiko linashuka kikamilifu.

Mawaziri ambao wapo katika subira ya wananchi kufuatia kauli zao ni wale ambao wameshaongea na vyombo mbalimbali vya habari na kudos maonyo au maelekezo kuhusu wajibu wa wizara walizoteuliwa kuzitendea kazi.

Waziri John Magufuli.
Baadhi ya wananchi walioongea na gazeti hili kwa nyakati tofauti walionesha wasiwasi wao kuhusu kauli hizo lakini wakasema kama safari hii wakuu hao wa wizara watakuwa wamebadilika basi JK atamaliza ngwe yake ya mwisho kwa kifua mbele.
KAULI ZAO:

Waziri John Magufuli; Yeye anashika Wizara ya Ujenzi ambapo ameanza kutema cheche zake. Miongoni mwa cheche hizo ni ile kauli yake ya kudos miezi sita kwa Manispaa za Jiji la Dar kumaliza tatizo la fileni.

Anna Tibaijuka; (pichani) Huyu mama anawajibika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. 

Waziri Anna Tibaijuka.
Alipoongea na waandishi wa habari alisema wale wote waliovamia maeneo ya wazi (ambayo ni mali ya Serikali) na kujenga wajisalimishe mara moja wizarani kwake kabla hawajasakwa.

William Ngeleja; Yeye anashikilia Wizara ya Nishati na Madini. Alipoongea na wanahabari alisema hakutakuwa na mgawo wa umeme nchini Tanzania.

David Mathayo; Amekabidhiwa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Jumapili iliyopita alitia timu Machinjio ya Dar iliyopo Vingunguti jijini Dar na kuchumba mkwara kuwa, anatoa mwezi mmoja (Januari mwakani) kwa Manispaa ya Ilala kuweka kila kitu sawa mahali hapo la sivyo, ohoo!

Waziri David Mathayo.
Utekelezaji wa kauli hizo unasubiriwa kwa hamu na wananchi nchini kote hasa wakizingatia kuwa, baadhi ya viongozi wa serikali siku za nyuma waliwahi kutoa maelekezo ambayo hayakutendewa kazi.

Afande Tibaigana; Akiwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, aliwahi kutoa tamko kuwa, daladala ni marufuku kusimamisha abiria akitaka watu wa kukaa tu (levo siti) maelekezo ambayo yalifanya kazi kwa muda mfupi na hali kurejea kama zamani hadi leo.

Yusuf Makamba; Akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam aliwahi kuchumba mkwara wa daladala zinazoingia kwenye vituo vya mafuta kujaza bidhaa hiyo huku zikiwa na abiria ndani. Agizo hilo lilidumu kwa muda mfupi na kurudia hali yake mpaka leo.

Waziri William Ngeleja.
Hata hivyo, Rais JK ameshasema atakuwa mkali na kiongozi ambaye atashindwa kusimamia majukumu yake.

Sitta afyatuka • ADAI DOWANS NI GENGE LA ULAJI WA VIGOGO WATATUWAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema ametishwa na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), iliyoipa ushindi Kampuni ya Dowans dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), lakini akasema haya ni matokeo ya genge la watu wachache wanaofahamika ambao wameamua kutafuna rasilimali za taifa bila huruma.
Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano katika miaka mitano iliyopita na ambaye aliruhusu Bunge kujadili masuala kashaa ya kifisadi,  Endelea kusma habari hii...

Muasisi wa Wikileaks akamatwa London

Muasisi wa mtandao wa Wikileaks Julian Assange amekamatwa mjini London.
Julian Assange
Julian Assange
Polisi wamesema Bw Assange ambaye anasakwa na Sweden kuhusiana na tuhuma za ubakaji alikamatwa siku moja baada ya kutolewa kwa hati ya kumkamata.
Bwana Assange anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.
Mtandao wa Wikileaks umekuwa ukichapisha taarifa za siri za mawasiliano ya ubalozi wa Marekani katika nchi mbalimbali jambo ambalo limeikasirisha na kuiaibisha Marekani.

Awali wakili wa Assange, Mark Stephens aliiambia BBC, alikuwa tayari kuzungumza na polisi wa Uingereza lakini haviamini vyombo vya sheria za Sweden.
Wakili huyo alisema hajaridhishwa na jinsi waendesha mashtaka wa Sweden wanavyochukulia kesi hiyo, kwa kuwa hawajamwambia Bw Assange ni ushahidi upi wanao dhidi yake.
Mbali na hayo wakili huyo amesema taarifa zaidi za siri zitachapishwa na Wikileaks.

Marekani yamtaka Gbagbo kung'atuka

Rais Gbagbo wa Ivory Coast
Marekani imemtaka rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, kukubali kuwa alishindwa katika uchaguzi wa hivi maajuzi na kumkabidhi madaraka mpinzani wake, Alassane Ouattara.
Afisa mmoja wa ikulu ya White House amesema rais Obama anamzingatia kuwa Bwana Ouattara ndiye aliyeshinda uchaguzi huo kihalali.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini,Thabo Mbeki, anatarajiwa kuwasilisha ripoti kwa umoja wa Afrika baada ya siku mbili za kujarbu kusuluhisha mgogoro huo nchini Ivory Coast.
Jumuiya ya kiuchumi kwa mataifa ya Afrika magaribi ECOWAS ambayo pia imemtangaza bwana Ouattara kuwa mshindi, inatarajiwa kuandaa mkutano maalum hivi leo Jumanne nchini Nigeria.
Jana Jumatatu, umoja wa mataifa ulisema unawaondoa japo kwa muda yapata wafanyikazi wake 500 wanaotoa huduma zisizokuwa za lazima kutoka nchini Ivory Coast kutokana na mzozo huo.

Dk Shein asita kuapisha majajiRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein amekuwa akisitasita kuwaapisha majaji wanne aliowateua Novemba 29 mwaka huu kufuatia barua aliyoandikiwa na Chama Cha Mawakili Zanzibar (ZLS) juu ya uteuzi huo kutozingatia taratibu.

Kusita huko kwa Dk Shein kuwaapisha tangu awateue kunaelezwa kuwa kunatokana na utata wa kisheria uliopo kutokana na majaji hao kutoiva vya kutosha katika taaluma ya sheria na kwa mujibu wa sheria tume ya utumishi ilipaswa kukaa kuidhinisha majina hayo jambo ambalo halikufanywa kwa baadhi ya majaji walioteuliwa.

Baadhi ya mawakili wakiongozwa na rais wa chama cha mawakili Zanzibar, Yahya Khamis Hamad waliosaini barua ya kumpinga Dk Shein juu ya uteuzi wa majaji hao ambao kwa mujibu wa maelezo yao hawana sifa zinazowafanya wawe majaji wa mahakama kuu.

Rais wa Zanzibar kwa mamlaka aliyopewa alifanya uteuzi wa majaji wanne wa Mahakama Kuu pamoja na Mwenyekiti wa Mahkama ya Ardhi ambaye ni Haroub Sheikh Pandu, na majaji wanne wa mahakama kuu akiwemo Abdul-hakim Ameir Issa, Fatma Hamid Mahmoud, Mkusa Isaac Sepetu, na Rabia Hussein Mohammed.

Chama hicho kilisema uteuzi huo, ulikuwa unatumia mamlaka aliyopewa rais na Katiba ya Zanzibar, 1984 kifungu cha 94(2) na (3) ambapo Chama cha Mawakili hakina mashaka na uteuzi wa Abdul-hakim Ameir Issa, wala uteuzi wa Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi, Haroub Shehe Pandu.

Chama hicho kilisema kuwa mashaka yapo kwa Fatma ambaye ni mtoto wake Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mkusa Isaac Sepetu na Rabia Hussein Mohammed ambao wote watatu wanadaiwa kutokuwa na sifa zinazostahiki kuteuliwa nafasi hiyo.

Juzi Disemba tatu usiku Jaji Mkuu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud aliitisha kikao cha tume ya utumishi ambacho anadaiwa kuwa hakikupitisha jina moja la jaji aliyeteuliwa na mawakili hao ili wajadiliane, lakini kikao hicho kilishindwa kufanyika baada ya kupokea barua nyengine kutoka chama cha mawakilishi kusema kwamba kikao kitakachofanyika hakitokuwa halali kwa mujibu wa sheria kwa kuwa wajumbe wa kikao hicho hawakutimia.

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na katibu wa chama cha mawakili, Salim Mkonje iliyotumwa kwa rais wa Zanzibar ya Desemba tatu mwaka huu, ambayo tayari saini ya rais inaonesha ameshaipokea ilisema kwamba wakili Awadh Ali Said ambaye alikuwa mjumbe wa tume ya uajiri anayetokana na chama hicho katika vipindi viwili vimekwisha tokea septemba 17 mwaka huu hivyo hawezi kuwa mjumbe tena hadi hapo atakapoteuliwa tena.

Mbali na mjumbe huyo, lakini pia Jaji Mshibe Ali Bakari naye muda wake umekwisha kwa mujibu wa sheria ya tume hiyo No 13 ya mwaka 2003 koramu ni wajumbe watano kifungu cha 9(2).

“Kufutia kikwazo hiki wakili Awadh alifahamishwa na katibu wa tume ya uajiri ya mahakama asihudhurie kikao cha leo 3 Desemba jana usiku” ilisema barua hiyo kutoka kwa mawakili. Na kuongeza kwamba.

“Kwa sababu wajumbe waliokuwepo walikuwa sita hivyo kupungua kwa wajumbe wawili kunapelekea tume isiweze kufanya maamuzi kama sheria inavyotaka kwani yatakuwa batili kwa kukosekana koram,” alisema barua hiyo.

Aidha chama hicho kimeitisha kikao chake jana kuteuwa jina la wakili ambaye atakiwakilisha chama hicho na kulipeleka kwa rais ili ateuliwe kuingia katika kikao hicho ikiwa pamoja na wajumbe wengine ambao sheria inasema tume hiyo iwe na wajumbe wanane akiwemo jaji mkuu, mwanasheria mkuu na mwenyekiti wa tume ya utumishi, na kadhi mkuu.

Serikali: Tuko tayari kukaa mezani na Chadema
SERIKALI imesema iko tayari kukaa meza moja na chama cha upinzani cha Chadema au taasisi nyingine yoyote itakayotaka kujadiliana kuhusu mustakabali wa taifa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira alisema kuwa serikali iko tayari kwa mazungumzo hayo iwapo yataweka mbele maslahi ya taifa.

Kauli ya Wassira imetolewa wakati Chadema ikiendelea na msimamo wake wa kutoyatambua matokeo ya uchaguzi wa urais, ikitaka kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza utangazaji wa matokeo hayo; kuandikwa kwa katiba mpya na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.

Chadema, ambayo ilitangaza msimamo huo mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu, ilithibitisha kwa vitendo kauli hiyo wakati wabunge wake walipotoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akianza kukihutubia chombo hicho.

Baadaye, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kuwa chama hicho kiko tayari kukaa meza moja na serikali au taasisi yoyote kujadili suala hilo kwa kuzingatia maslahi ya taifa.


Lakini katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alibeza kauli hiyo ya Mbowe kwa kusema kuwa chama hicho tawala hakina muda wala sababu ya kuketi pamoja na wapinzani hao na kwamba baada ya rais kupatikana, siasa sasa zinahamia bungeni.

Jana Waziri Wassira alitoa kauli tofauti na ya katibu wake mkuu alipoiambia Mwananchi kuwa wako tayari kukaa meza moja na Chadema, chama au taasisi yoyote ikiwamo za dini na kwamba mazungumzo watayoyalenga ni yale yatakayohakikisha yanaweka mbele maslahi ya taifa.

“Lakini nasisitiza serikali haina mgogoro na viongozi wa dini au chama chochote bali milango ipo wazi kwa vyama vyote 18 na taasisi zote," alisema waziri huyo ambaye aliwahi kuwa kwenye upinzani baada ya kuihama CCM na kujiunga na NCCR-Mageuzi miaka ya tisini.

"Majadiliano yasichukue sura ya kisiasa au udini kwa kuwa kufanya hivyo hakutafanikisha kufikiwa kwa maslahi bora ya baadaye ya nchi.

“Lengo la serikali ni kuhakikisha taifa hili linalifikishwa mahali ambapo amani na utulivu itaendelea kuwepo.”
Hata hivyo, Waziri huyo alisema kama kutatokea matatizo au kutoelewana, serikali ina njia na taratibu zake inazozitumia kukutana na walengwa kutatua hali hiyo na kwamba hatua hizo huwa hazitangazwi kwenye vyombo vya habari.

Wakati akifafanua msimamo huo wa Chadema kwa waandishi wa habari, Mbowe alisema mazungumzo watakayoyalenga ni yale yatakayohakikisha kuwa madai yao yanafikiriwa kwa kina huku maslahi ya taifa yakiwekwa mbele.

Mbowe alisema wanafurahi kuona kuwa kitendo chao cha kutoka bungeni wakati wa hotuba ya Rais Kikwete kimesaidia kuibua mjadala mzito nchini ambao iwapo utapewa nafasi ya kujadiliwa bila kuweka ushabiki wa kisiasa, nchi inaweza kupata mabadiliko makubwa siku za usoni.

Alitoa mfano kauli ya waziri mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba na Jaji Mkuu Augustino Ramadhani ambao walikaririwa wakisema kuwa suala la katiba mpya ni muhimu.

“Maoni kama haya, ambayo yanatoka kwa watu wazito kama hawa, yanaonyesha kuwa kitendo chetu kimeamsha mjadala wa maana kwa taifa hili,” alisema.

Chadema, ambayo ilionekana kama haingesimamisha mgombea urais baada ya Mbowe kuamua kugombea ubunge wa Jimbo la Hai, iliibukia kuwa mpinzani mkuu wa CCM baada ya kumtangaza mbunge wa zamani wa Karatu, Dk Willibrod Slaa kuwa mgombea urais.

Dk Slaa, ambaye alikuwa akivutia maelfu ya watu kwenye mikutano yake ya kampeni ambako alikuwa akihubiri elimu ya bure na upunguzaji wa bei za vifaa vya ujenzi, alitangaza kutokubaliana na mwenendo wa utangazaji matokeo ya uchaguzi wa rais na kuitaka Tume ya Uchaguzi (Nec)kusimamisha zoezi hilo.

Lakini Nec iliendelea na utangazaji matokeo na baadaye kumtangaza Jakaya Kikwete kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais, tamko ambalo liliifanya Chadema kutangaza msimamo wake wa kutotambua matokeo ya uchaguzi wa rais.

Wahisani:Bajeti tuliyopewa ni tofauti na ile iliyosomwa Bungeni

Waziri wa Fedha na Uchumi ,Mustapha Mkulo akizungumza na wandishi wa habari Dar es Salaam jana, baada ya kumalizika kwa mkutano wa kitaifa wa mwaka wa majadiliano ya kisera na bajeti. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimafaifa (IMF) hapa nchini John Wakeman-Linn

KUNDI la wahisani wanaochangia bajeti kuu ya Tanzania (GBS) limeibua kashfa baada ya kueleza kuwa serikali iliwapelekea bajeti tofauti na ile iliyopitishwa na Bunge Julai mwaka huu.Taarifa za kashfa hiyo ziliwekwa hadharani jana asubuhi na mwenyekiti wa wahisani hao, Svein Baera wa Sweden katika mkutano wa kitaifa wa mwaka wa majadiliano ya kisera na bajeti uliofanyika jijini Dar es salaam.

Sweden ndiyo inayoshikilia uenyekiti wa kundi hilo linalojumuisha taasisi za kimataifa na nchi mbalimbali zilizoendelea.

Kuibuliwa kwa kashfa hiyo kunakuja wakati wahisani hao wakiwa wamezuia theluthi moja ya zaidi ya dola 800 milioni za Kimarekani ambazo zinatakiwa zichangie kwenye bajeti kuu ya 2010/11, wakiishinikiza serikali iharakishe utekelezaji wa programu ya mageuzi, yakiwemo ya mfumo wa usimamizi wa fedha za seikali.

Akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo wa siku tatu, Baera aliainisha maeneo sita kuwa ndiyo mhimili wa mjadala wao na serikali.

"Napenda kuainisha maeneo sita ya ujumbe wetu ili kuweka sawa jukwaa la majadiliano yetu haya ya mwaka. Kuna tofauti kati ya bajeti iliyowasilishwa kwa bodi ya (Shirika la Kimataifa la Fedha) IMF na ile iliyopitishwa na Bunge Julai 2010," alisema Baera.

Alisema bajeti ambayo serikali iliwasilisha kwa wahisani hao ilibeba "matumaini makubwa ya kuzaa matokeo mazuri na kufanywa kama sababu ya kupitisha matumizi makubwa ya fedha zitokanazo na mapato ya ndani".
Baera alisema kuwa kukosekana kwa uwazi katika matumizi, vipaumbele, mapato na mfumo mzima wa fedha kunapunguza kuaminika kwa bajeti hiyo mbele ya wafadhili.

Kwa mujibu wa wahisani hao, kumekuwepo na mtiririko wa athari katika bajeti katika miaka ya karibuni huku ikionyesha ongezeko kubwa la matumizi ya kawaida kuliko yale ya maendeleo.

Kwa mujibu wa bajeti ya mwaka 2010/11 ambayo ni ya Sh11.1 trilioni, matumizi ya kawaida ya serikali ni Sh7.8 trilioni wakati fedha zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo ni Sh3.2 trilioni.

Bajeti hiyo inaonyesha kuwa kati ya Sh11.1 trilioni, serikali ilitarajia kupata Sh6 trilioni kutoka katika vyanzo vya ndani, wakati inatarajia Sh2.8 trilioni kutoka kwa wahisani na mikopo. Fedha nyingine zinatarajiwa kutoka mikopo ya ndani, masharti ya kibiashara na ubinafsishaji.

"Matumaini makubwa kupindukia katika bajeti hii na kutokuwepo kwa mikakati inayoeleweka ya kipaumbele katika matumizi katika hali inayoweza kutokea ya mapato madogo na ukosefu wa fedha, yanaweza kuondoa kuaminika kwa bajeti kama chombo cha ufanisi wa sera na mipango," alisema Baera.

Zaidi ya hapo, ukweli kwamba bajeti hii tofauti ilipitishwa bila ya kuwepo mawasiliano ya awali na wabia wa maendeleo inaweka maswali kwenye ubora wa mazungumzo yetu ya sera na ubia. Tunatarajia kujadili suala hili kwenye sehemu muhimu ya bajeti.

"Zaidi ya hapo, bajeti iliyotumiwa kuanzia mwaka jana iliendeleza mwenendo wa miaka ya karibuni ambako matumizi ya kawaida yanaendelea kupanda kwa kasi kuliko matumizi kwenye maendeleo."

Kutokana na hali hiyo GBS imeitaka serikali kujipanga upya na kuweka mkazo katika kupunguza misamaha ya kodi ili kuweka uwiano na ufanisi sawa na nchi za kundi lake katika uchumi, hatua ambayo Baera alisema itapunguza pengo la bajeti linaloikabili Tanzania kila mwaka.

Tayari GBS imebainisha kuwa bajeti ijayo inaweza kuwa na nakisi ya hadi Sh1 bilioni.
Hata hivyo, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo ambaye alishiriki mkutano huo, alipatwa na kigugumizi kujibu madai hayo ya GBS, akimkaribisha mwenyekiti huyo wa kundi la nchi wahisani aende ofisini kwake ili wazungumzie masuala hayo.

"Kuna mengine yanazungumzika; Baera ninakukaribisha ofisini kwangu; mengine yanazungumzika ofisini," alisema Mkulo.

Naibu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Zitto Kabwe alizungumzia kasoro hiyo jana akieleza kuwa imemshtua na kwamba ataifuatilia.

Zitto, ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini na ambaye alihudhuria mkutano huo jana, alisema kambi ya upinzani itaunda kamati kulifuatilia suala hilo.

Alisema pia watahoji suala hilo bungeni na kuitaka serikali iweke wazi kwa Watanzania ni bajeti ipi inayotumika kati ya iliyopitishwa na Bunge na ile iliyopelekwa IMF.

"Huu ni mshtuko kwangu; hili limenishtua. Tutaunda timu ya kulifuatilia; tutalifikisha bungeni na kuihoji serikali ieleze ni bajeti ipi inayotumika. Ni ile iliyopitishwa na Bunge au iliyopelekwa IMF," alisema Zitto.

Kundi hilo la nchi wahisni limesema kuwa linaunga mkono mkakati wa serikali wa Kilimo Kwanza na wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu maendeleo ya kilimo, hifadhi ya chakula na kupunguza umasikini.

AIBU BOSI WA BANDARI AFUMWA AKILA URODA


Na Mwandishi Wetu
Ofisa Mwandamizi Uchukuzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Makao Makuu jijini Dar, Kitengo cha Makontena, Peter Milanzi (54) amejikuta ndani ya aibu nzito kufuatia madai kwamba, amekutwa akiwa na mke wa mtu kwenye nyumba ya kulala wageni ‘gesti hausi’, Ijumaa Wikienda linashuka na ‘diteilzi’. 

Tukio hilo lililoacha historia, lilijiri Desemba Mosi, 2010 (Siku ya Ukimwi Duniani) majira ya alasiri kwenye chumba namba tano cha hoteli moja (jina tunalo), Buguruni, Dar.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mume aliyejitambulisha kwa jina la Shaha Juma alidai kumbamba Milanzi akiwa na mkewe wa ndoa aitwaye Salia.

Chanzo hicho kikaongeza kudai kuwa, kabla ya fumanizi hilo lililokusanya mashuhuda kibao, mume wa mwanamke huyo alikuwa na kibarua kizito cha kufuatilia nyendo za ‘wezi’ hao mpaka ndani ya chumba hicho. Endelea kusoma habari hii...