IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:

Kuna habari kwamba baadhi ya vigogo wa Jeshi la Polisi na mfanyabiashara mmoja waliotajwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Mzee Reginald Abraham Mengi watafikishwa mahakamani kwa madai ya kutaka kumbambikizia mwanae dawa za kulevya.
Habari zilizopatikana kutoka vyanzo vyetu vya habari ndani ya jeshi la polisi vimedai kuwa, vigogo hao watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa ili haki iweze kupatikana.

Taarifa hizo zimedai kuwa uhamisho wa vituo vya kazi uliofanywa ndani ya jeshi hilo ambapo Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kanda Maalum, jijini Dar es Salaam, Charles Mkumbo wamehamishiwa makao makuu ya jeshi hilo, ni mpango mahususi wa kutoa fursa kuwafikisha kortini ili tuhuma zao zikaamuliwe na chombo hicho.
“Uhamisho uliofanywa ndani ya jeshi siyo wa kawaida kwani hata maofisa wengine waliohamishwa wamefanyiwa hivyo ili kufunika hili la watuhumiwa wa
Endelea....
0 comments:
Post a Comment