Udini ni ulaji wa wakubwa – Warioba

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

WAZIRI Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba amesema udini unaotajwa kuwapo nchini, hasa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, umo miongoni mwa viongozi si wananchi wa kawaida.
Kauli hiyo ya Jaji Warioba ni sehemu ya maoni yake ya maadhimisho ya miaka 49 ya Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika, Desemba 9, mwaka 1961 yanayofanyika kesho Alhamisi.

Amesema licha ya viongozi waasisi kufanikiwa kujenga Taifa moja, dalili za sasa si njema na kwamba kasi ya viongozi kugawanyika hata katika vyama vyao vya siasa inaelekea kutishia umoja wa nchi.

Katika mahojiano maalumu na Raia Mwema yaliyochapishwa katika kurasa za tisa na 10 za toleo hili, Jaji Warioba anasema wananchi kawaida wamekuwa wakiendelea na shughuli zao bila kuulizana dini wala kabila zao.

“Wanafanya shughuli zao za kawaida iwe za biashara au uzalishaji. Ukikuta kundi la Wamachinga utawakuta vijana wa kutoka sehemu mbali mbali, dini mbali mbali na kabila mbali mbali wanafanya shughuli moja, hawajibagui hata kidogo.

“Inapofika wakati wa uchaguzi ndipo unasikia haya mambo ya ukabila, ukanda na udini. Haya yanaletwa na hawa ambao wanatafuta madaraka. Hawa wanaotafuta madaraka ndio wameleta matumizi ya fedha katika kutafuta uongozi,” alisema Jaji Warioba.

Katika hatua nyingine, Jaji Warioba ambaye amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere, ameonyesha kukerwa na tabia mpya ya kutojiamini kama nchi kiasi cha kutegemea zaidi wafadhili.

“Kwa nini waasisi wetu walijiamini zaidi kuliko sasa hivi? Mimi nadhani wakati ule TANU inadai Uhuru tukiwa vijana ndiyo tumeingia kwenye siasa, hali ilikuwa ngumu sana. Endelea Kusoma Habari Hii..

0 comments: