Sitta: Kuilipa Downs ni kuhujumu uchumi

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter ASEMA HIZO NI NJAMA ZA GENGE LINALOTAFUTA FEDHA ZA UCHAGUZI MKUU 2015
WAZIRI mpya wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri, amesema hatua yoyote ya kulipa fidia ya Sh 185 bilioni kwa kampuni ya Dowans, ni kuhujumu uchumi wa nchi.

Sitta, ambaye aliongoza Bunge la Tisa lililotikisa nchi kwa kuibua kashfa za ufisadi, pia amesema kuna kila dalili za genge linalohujumu nchi kuandaa mpango wa kutafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.

Sitta alikuwa akitoa maoni yake baada ya kuulizwa na Mwananchi kuhusu hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuhishi wa Kibiashara (ICC) iliyolitaka Shirika la Umeme (Tanesco) kuilipa Dowans Sh185 bilioni kutokana na kuvunja mkataba bila ya kufuata taratibu.

Tanesco ilivunja mkataba huo wa kuzalisha umeme mwaka 2008, ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya kuisha, ikieleza kuwa mkataba huo ulikiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma. Tanesco imesema itazungumzia suala hilo baada ya hukumu hiyo kusajiliwa nchini.

0 comments: