Mawaziri Hawa Wanajaribu Kuipa Nchi Hadhi Yake

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Kitendo cha baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya JK ambao wametoa kauli za utendaji mara baada ya kuapishwa zimechukuliwa na wananchi kama ni kitanzi kwao endapo maelekezo yao hayatakamilika, Risasi Mchanganyiko linashuka kikamilifu.

Mawaziri ambao wapo katika subira ya wananchi kufuatia kauli zao ni wale ambao wameshaongea na vyombo mbalimbali vya habari na kudos maonyo au maelekezo kuhusu wajibu wa wizara walizoteuliwa kuzitendea kazi.

Waziri John Magufuli.
Baadhi ya wananchi walioongea na gazeti hili kwa nyakati tofauti walionesha wasiwasi wao kuhusu kauli hizo lakini wakasema kama safari hii wakuu hao wa wizara watakuwa wamebadilika basi JK atamaliza ngwe yake ya mwisho kwa kifua mbele.
KAULI ZAO:

Waziri John Magufuli; Yeye anashika Wizara ya Ujenzi ambapo ameanza kutema cheche zake. Miongoni mwa cheche hizo ni ile kauli yake ya kudos miezi sita kwa Manispaa za Jiji la Dar kumaliza tatizo la fileni.

Anna Tibaijuka; (pichani) Huyu mama anawajibika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. 

Waziri Anna Tibaijuka.
Alipoongea na waandishi wa habari alisema wale wote waliovamia maeneo ya wazi (ambayo ni mali ya Serikali) na kujenga wajisalimishe mara moja wizarani kwake kabla hawajasakwa.

William Ngeleja; Yeye anashikilia Wizara ya Nishati na Madini. Alipoongea na wanahabari alisema hakutakuwa na mgawo wa umeme nchini Tanzania.

David Mathayo; Amekabidhiwa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Jumapili iliyopita alitia timu Machinjio ya Dar iliyopo Vingunguti jijini Dar na kuchumba mkwara kuwa, anatoa mwezi mmoja (Januari mwakani) kwa Manispaa ya Ilala kuweka kila kitu sawa mahali hapo la sivyo, ohoo!

Waziri David Mathayo.
Utekelezaji wa kauli hizo unasubiriwa kwa hamu na wananchi nchini kote hasa wakizingatia kuwa, baadhi ya viongozi wa serikali siku za nyuma waliwahi kutoa maelekezo ambayo hayakutendewa kazi.

Afande Tibaigana; Akiwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, aliwahi kutoa tamko kuwa, daladala ni marufuku kusimamisha abiria akitaka watu wa kukaa tu (levo siti) maelekezo ambayo yalifanya kazi kwa muda mfupi na hali kurejea kama zamani hadi leo.

Yusuf Makamba; Akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam aliwahi kuchumba mkwara wa daladala zinazoingia kwenye vituo vya mafuta kujaza bidhaa hiyo huku zikiwa na abiria ndani. Agizo hilo lilidumu kwa muda mfupi na kurudia hali yake mpaka leo.

Waziri William Ngeleja.
Hata hivyo, Rais JK ameshasema atakuwa mkali na kiongozi ambaye atashindwa kusimamia majukumu yake.

0 comments: