Watu walioshuhudia wamesema kuwa hali ya kukanyagana ilianza baada ya watu kadhaa kuuawa kwa umeme katika daraja dogo lililokuwa na taa zinazounganisha mji wa Phnom Penh kwenda kisiwa cha karibu ambako maelfu ya watu walikusanyika kusherekea sikukuu ya maji na kuangalia matamasha.
Watu wengi walikufa kutokana na kuzama, kukosa hewa au kukanyagana wakati walipojaribu kuondoka katika daraja hilo. Mamia ya watu wengine walijeruhiwa katika maafa hayo, ambayo Waziri Mkuu wa Cambodia Hun Sen, ameyaita mauaji makubwa kutokea nchini humo katika miongo kadhaa.
0 comments:
Post a Comment