
Chuo Kikuu Cha Dodoma leo kimewatunuku Shahada ya Heshima ya
Udaktari (Doctor Honoris Causa) Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa kwa kutambua michango yao mbalimbali katika Nyanja za siasa na sekta za elimu nchini ikiwemo kuasisi ujenzi wa Chuo hicho. Pichani ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, akimtunuku shahada ya Heshima ya Udaktari Rais Dr.Jakaya Kikwete wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo hicho iliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma leo. Katikati ni Makamu mkuu wa Chuo Profesa Idriss Kikula
0 comments:
Post a Comment