Dkt Robert Ouko 'aliuwawa ikulu

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Bunge la Kenya. Ripoti ya mauaji ya Dkt. Ouko ilitayarishwa miaka mitano iliyopita na kuwasilishwa bungeni jana Jumatano.
Ripoti iliyotarishwa na kamati ya bunge la Kenya miaka mitano iliyopita imedai kuwa aliyekuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni aliyekuwa na ushawishi mkubwa Robert Ouko, aliuwawa katika ikulu ya rais mjini Nakuru.
Ripoti hiyo iliyotayarishwa na kundi la wabunge wa Kenya inadai kuwa Bwana Ouko aliuwawa baada ya kutofautiana na waziri mwenzake katika serikali ya rais mustaafu Daniel Arap Moi wakiwa ziarani nchini Marekani.
Ripoti hiyo iliwasilishwa katika bunge la Kenya siku ya Jumatano. Ripoti hiyo inapendekeza kuchunguzwa kwa watu mashuhuri waliohudumu katika serikali ya rais mustaafu Daniel Arap Moi, wanaodaiwa kuhusika katika mauaji ya bwana Ouko.
Rais Mustaafu wa Kenya Daniel Arap Moi. Dkt. Robert Ouko aliuwawa wakati wa utawala wake.
Kadhalika ripoti hiyo inadai kuwa Bwana Ouko aliyeuwawa mwaka 1990, alikuwa tayari amefutwa kazi na walinzi wake kuondolewa juma moja kabla ya kutoweka kwake.
Ripoti hiyo inadai kuwa ubishi uliibuka kati ya Bwana. Ouko na waziri mwenzake baada ya waziri huyo kumkejeli kwa kumwita Ouko ''Bwana Rais''.
Mauaji ya Bwana Ouko yalizua tetesi kali nchini Kenya na ni mojawepo tu ya mauaji mengi ya kisiasa yanayodaiwa kutekelezwa na serikali ya Kenya tangu taifa hilo lijinyakulie uhuru mwaka 1963.
Uchunguzi wa kina wa mauaji hayo bado haujakamilika huku mfumo wa sheria nchini humo ukilaumiwa kwa kuwa kizingiti cha kupatikana ukweli.

0 comments: