Balozi Mbita ataka mabadiliko ya Katiba

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
















BALOZI Hashim Mbita ambaye alikuwa Katibu wa Kamati ya Ukombozi ya uliyokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) amewashangaa wanasiasa wanaoogopa kuifanyia mabadiliko katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza katika Televisheni ya Taifa jana asubuhi, Balozi Mbita alisema: “Katiba yetu ina ukakasi, hivyo inahitaji kufanyiwa mabadiliko ili iweze kwenda na wakati na mfumo wa kisiasa ulipo sasa na kudumisha umoja wa kitaifa”.

Alifafanua kuwa katiba iliyopo inaweka sera za maendeleo mikononi mwa wahisani ambao huamua hatima ya nchi, hivyo kuzorotesha juhudi za maendeleo.

Balozi Mbita alitoa mfano kuwa wafadhili walishawahi kukataa utekelezaji wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria mpaka mkoani Shinyanga kwa kuwa haukuwa katika vipaumbele vyao.

Kauli hiyo ya Mbita inakuja wakati kumeibuka mjadala mkali katika jamii kwa wanaharakati na vyama vya upinzani vitaka mabadiliko ya katiba huku viongozi wa chama tawala wakiwemo wabunge na mawaziri wakipinga hatua hiyo.
Hivi karibuni, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Celina Kombani alisema katiba haiwezi kubadilishwa na kwamba hajui madai ya wapinzani kuhusu yanahusu nini na kwamba hawezi kushghulikia kwa vile hajapelekewa rasmi maelezo ya mambi yanayotakiwa kubadilishwa.

Wabunge wa Chadema walisimama na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kusima ili kutoa hotuba ya kufunga rasmi Bunge la kumi la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania wakidai kuwa hawakubaliani na katiba iliyomweka madarakani kwa kuwa ina kasoro nyingi.

Kitendo hicho kiliamsha changamoto mpya katika jamii ya Watanzania wakiwemo vijana na wasomi ambao wanasema sasa umefika wakati wa kuifanyia mabadiliko Katiba kwa manufaa ustawi taifa.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Gaudence Mpangala, ambaye alishiriki katika kipindi hicho cha TBC alisema katiba mpya italinufaisha taifa kwa kuboresha misingi ya uongozi bora na siasa safi nchini kwa sababa iliyopo sasa haiendi na wakati, mfumo wa siasa na sera za taifa.

0 comments: