KASHFA ya sanya sanya ya viwanja katika maeneo muhimu nchini imezidi kushamiri ikiwahusisha waliokuwa mawaziri pamoja na familia zao akiwemo pia mtoto wa Rais Kikwete, Ridhiwan Kikwete, Raia Mwema limebaini.
Uchunguzi wa Raia Mwema katika baadhi ya maeneo nchini, ikiwamo mikoa ya kanda ya Kaskazini, Dar es Salaam na mkoa wa Pwani, unaonyesha kwamba vigogo hao wamekuwa wakijitwalia maeneo kwa kasi ya ajabu; huku wenyeji wa maeneo hayo wakinyimwa.
Kwa mujibu wa habari hizo, baadhi ya maeneo vigogo hao wamekuwa wakinunua kwa fedha taslimu na baadhi ya maeneo wamekuwa wakijitokeza na kugawiwa na watendaji wa halmashauri na manispaa za maeneo husika; huku maelfu ya wananchi wa maeneo husika wakinyimwa pamoja na kuwa wa mwanzo kuomba na kulipia gharama za fomu ambazo hutumika kupimia viwanja.
Mfano wa hivi karibuni ni mkoani Arusha ambako siku chache baada ya uchaguzi mkuu, vigogo kadhaa waligawiwa viwanja katika mazingira tata huku maelfu ya wananchi wa mkoa huo walioomba wakijikuta wakiwa hawamo katika orodha ya watu waliopata viwanja iliyobandikwa kwenye ubao wa matangazo na kubanduliwa baada ya wananchi kuanza kulalamika.
Sakata hilo la aina yake limetokea katika Halmashauri ya Arusha Vijijini mkoani Arusha ambako Idara ya Ardhi ya Halmashauri hiyo ilikusanya mamilioni ya fedha kutoka kwa wananchi, wakiwemo ‘makabwela’, kwa ajili ya kupimiwa viwanja katika eneo la Burka ambavyo hata hivyo vimegawiwa kwa vigogo.
Mbali ya Ridhiwan, vigogo wengine waliogawiwa viwanja vya Burka huko Arusha Vijijini ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Phillip Marmo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Aggrey Mwanri.
Mnamo Agosti mwaka huu, Halmashauri ya Arusha Vijijini ilitangaza kuwa itagawa viwanja katika eneo hilo na wananchi waliokuwa wakivihitaji walipaswa kununua fomu kwa ada ya Sh. 10,000 kila mmoja na kujaza fomu hizo kisha kuzirejesha katika ofisi ya ardhi.
Kufuatia tangazo hilo, idadi kubwa ya wakazi wa wilaya hiyo na wale wa Arusha Mjini walimiminika katika ofisi za ardhi na kulipia ada ya fomu
ambapo zaidi ya watu 20,000 walijitokeza na kujaza fomu na kuzirudisha.
Katika makusanyo ya ada za fomu pekee Halmashauri hiyo inakadiriwa kuwa ilikusanya zaidi ya Shilingi milioni 300 katika kipindi cha siku nne tu za utoaji fomu kutoka kwa wananchi mbalimbali wakiwemo watu wenye uwezo mdogo kiuchumi.
Taarifa za uhakika zilizoifikia Raia Mwema zinasema kwamba halmashauri hiyo ilificha idadi ya viwanja makusudi kwa nia ya kuvuta watu wengi kadri itakavyowezekana ili kupata fedha za kupima viwanja hivyo kabla ya kuviuza.
Aidha, habari za ndani ya Halmashauri hiyo zilieleza kuwa wakati wakitangaza kugawa viwanja hivyo kamati ya ardhi na mipango miji haikuwa imepima viwanja hivyo kutokana na kutokuwa na fedha za kulipa wapimaji ambao walikuwa ni kutoka Chuo cha Ardhi.
“Badala yake kamati hiyo ilibuni mbinu za kuchukua fedha za malipo ya ada za fomu zilizochangwa na wananchi ambapo wataalamu wa chuo hicho walilipwa fedha zinazokaribia kufikia Sh. milioni 90 kwa kazi hiyo na zaidi ya Sh. milioni 200 zilizobakia kati ya 300 zilizopatikana na kwa mauzo ya ada za fomu ziliingia Halmashauri”, alieleza mtoa habari wetu.
Aidha imeelezwa kuwa wakati fedha hizo zikikusanywa kutoka kwa watu 20,000 waliojaza fomu, maofisa wa idara ya ardhi walikuwa wanafahamu fika kuwa katika eneo hilo kulikuwa na uwezekano wa kugawa viwanja visivyozidi 800 tu.
Habari zaidi zinaeleza kuwa kamati hiyo ilipanga makusudi kuyatangaza hadharani majina ya waliopata baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu kwani majina hayo yangetolewa kipindi cha kampeni za uchaguzi yangeathiri kura za wagombea wa CCM katika uchaguzi huo.
“Majina ya waliogawiwa yalitolewa baada ya uchaguzi mkuu kumalizika; kwani kamati ilibaini kuwa kutokana na mapungufu yaliyo kuwepo katika mradi huo ingeathiri sana matokeo ya uchaguzi hasa kwa upande wa CCM,” alibainisha mtoa taarifa wetu.
Baada ya waliojaza fomu ya kuomba viwanja hivyo kusubiri kwa muda wa miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu, Halmashauri hiyo ilitangaza majina ya waliofanikiwa kupata viwanja hivyo siku chache baada ya uchaguzi huo, Novemba 2 mwaka huu na kuyabandika katika mbao za matangazo za Halmashauri, na kwa mshangao wa wengi baadhi ya majina yaliyobandikwa yalikuwa ya viongozi, watendaji wa serikali nawafanyabiashara wakubwa.
Vigogo hao, hata hivyo, wengi ni wale wanaoishi nje ya mkoa wa Arusha; hali ambayo imezua malalamiko kutoka kwa wananchi walioomba viwanja hivyo kuwa maafisa wa Halmashauri hiyo wamehusika kuwalaghai fedha zao.
Lakini pia katika hali ya kushangaza watendaji wa Halmashauri hiyo walilazimika kuondoa baadhi ya majina ya vigogo hao katika ubao wa matangazo siku tatu baada ya kubandika majina kufuatia wananchi kulalamikia utaratibu mzima na vigezo vilivyotumika kuwapatia viwanja viongozi ambao wengi si wakazi wa Arusha.
Katika orodha iliyobandikwa awali, ambayo Raia Mwema ilifanikiwa kuinakili kabla haijaondolewa, jina la Ridhiwan Jakaya Kikwete limefuatana na lile la aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Aggrey Mwanri ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro.
Wengine ni Sophia Simba ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) na pia alikuwa Waziri wa Utawala Bora, aliyekuwa Waziri wa Nchi anayeshulikia masuala ya Bunge na Sera, Philip Sanka Marmo ambaye pia alikuwa Mbunge wa Mbulu kabla ya kupoteza nafasi hiyo kwa mgombea wa CHADEMA katika uchaguzi uliofanyika wiki mbili zilizopita.
Vigogo wengine ni pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Benno Ndulu, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dk.Charles Stephen Kimei, Meneja wa Benki hiyo mkoani Arusha, Bi.Chiku Issa Athuman na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, John Ole Saitabau na Katibu Mkuu wa UWT mkoa wa Arusha Bi.Elly Minja.
Katika orodha hiyo pia wamo wakuu wa mikoa ambao ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Parseko Vicent Kone, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdori Leka Shirima na Mkurugenzi Mtendaji wa jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, mbunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ritha Mlaki na Mbunge wa Singida Vijijini, Lazaro Nyalandu (CCM).
Pia wamo watu wenye majina ambayo yana ubini unaofanana na viongozi maarufu na hao ni Frida Nyalandu ambaye habari zinaeleza kuwa ni ndugu wa mbunge Lazaro Nyalandu, Innocent Karamagi ambaye hata hivyo uhusiano wake na Nazir Karamagi haukuweza kufahamika mara moja, Andrew Lowassa, Hilary Ngoyai na Evance A.Ngoyai ambao pia uhusiano wao na aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa haukufahamika mara moja.
Hata hivyo, ugawaji huo “umewasha moto” wa malalamiko kutoka kila kona ya mji wa Arusha kutoka kwa makundi ya kijamii ambapo baadhi wanaiomba serikali kuingilia kati na kusitisha zoezi hilo na ugawaji uanze upya na vigezo vizingatiwe.
“Hakukuwa na vigezo katika zoezi la kuomba viwanja isipokuwa swali katika fomu ambalo liliuliza iwapo mwombaji anamiliki ardhi sehemu nyingine……kwa hiyo kwa kigezo hicho huwezi kunishawishi kuwa vigogo kama hawa (anawataja majina) hawamiliki ardhi sehemu nyingine,” alisema mmoja wa walalamikaji na kuongeza;
“Kwa ufahamu wangu hawa wanaweza kuwa wanamiliki ardhi nyingi tena katika maeneo nyeti (prime areas) hapa nchini. Naiomba serikali iingilie kati suala hilo fedha za watu maskini haziwezi kutumiwa kuwapimia viwanja vigogo,”alisema mwananchi huyo.
Akizungumzia malalamiko hayo na Raia Mwema kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Arusha Vijijini, Khalifa Hidda alikataa kulitolea ufafanuzi na kumtaka mwandishi afike ofisini kwake na kuonana naye uso kwa uso pamoja na kutopatikana tena baadaye.
Akizungumzia malalamiko hayo na mengine, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, alisema taarifa alizonazo ni kwamba viwanja vya Arusha viligawanywa kwa kufuata taratibu, lakini alikataa kuzungumzia kuhusishwa kwa vigogo.
"Habari nilizonazo ni kwamba viwanvya vya Burka huko Arusha walivigawa kufuata taratibu na sheria za ardhi. Kama kulitokea upendeleo na ukiukwaji wa taratibu na sheria, ofisi yangu haijapata taarifa. Tukipata taarifa, tutafuatilia na kuhakikisha wanaohusika na ukiukwaji huu wanachukuliwa hatua," alisema katika mahojiano na Raia Mwema.
Raia Mwema, hata hivyo, lilibaini kuwa hali ya vigogo kujitosa upya kwenye sanya sanya ya viwanja vilivyopo kwenye prime areas imejitokeza pia katika miji ya Dar es salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Tanga na maeneo kadhaa ya mkoa wa Pwani.

0 comments:
Post a Comment