Kauli hiyo, ilitolewa na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa jana.
Alisema chuo kinatarajia kufanya uzinduzi pamoja na miundombinu Novemba 25, mwaka huu, ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Rais Jakaya Kikwete.
Pamoja na uzinduzi huo, Profesa Kikula alisema Novemba 26, chuo kitaandika historia ya kwanza kwa kuwahitimisha wanafunzi 1,279 wa fani mbalimbali.
Alisema wanafunzi hao, watakuwa ni wahitimu wa kwanza katika chuo hicho na watatunukiwa shahada mbalimbali ikiwa ni pamoja na baadhi ya wanafunzi kuhitimu mafunzo ngazi ya cheti.
Alisema pamoja na kuwepo kwa wahitimu hao, chuo kimeamua kumuenzi muasisi na mpiganaji katika harakati za kutafuta uhuru, hayati Kawawa kwa kumtunukia shahada ya Heshima (Doctor of Honors Causa), ikiwa ni kumuenzi kwa juhudi zake za uanzishwaji wa chuo hicho.
Alisema, katika mahafali hayo Rais mstaaafu, Benjamini Mkapa pia atahudhuria pamoja na makatibu wakuu wa wizara mbalimbali.
Alisema chuo hicho, kitahakikisha elimu inayotolewa chuoni hapo inakuwa bora ambapo mpaka sasa wameweza kuajiri walimu 300, huku nusu yao wakipelekwa nje kwa ajili ya kupata elimu zaidi.
0 comments:
Post a Comment