Amesema suala la udini linapandikizwa na Rais Kikwete, hali ambayo inaweza kuvuruga amani ya nchi tuliyoizoea.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mtikila alisema Rais Kikwete anakiuka Katiba ya nchi kwa kutawala kwa kutumia udini kwa kuwapendelea Waislamu.
Aliendelea kusema kuwa dini zote zinatakiwa kuabudu lakini zisivunje Katiba lakini; Rais Kikwete anataka kuisilimisha nchi ili na kuingia Jumuiya ya Kiislamu (OIC).
Alisema kila Mtanzania angepiga kura kwa kufuata udini, Rais Kikwete asingeweza kushinda hata kama angechakachua matokeo hayo kutokana na Watanzania kujua kuwa dini ya aina moja si kigezo cha kumpata kiongozi bora.
“Rais Kikwete anazungumzia udini wakati Watanzania wanaamini kuwa viongozi hawachaguliwi kwa udini. Hili kwake la udini analitoa wapi au anataka kujenga taifa la dini fulani!?” alihoji Mchungaji Mtikila.
Mchungaji Mtikila alisema udini ni baruti ya hatari ya kupindukia, nchi zote zinazofaidi amani ya kweli na demokrasia zimepiga marufuku serikali zao kugusa suala la dini kabisa.
Alisema Rais Kikwete anakiuka Katiba ya nchi katika ibara ya 19 (2) kwani inaeleza kuwa kazi ya kufanya ibada na kueneza dini ni jambo la mtu binafsi na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.
Alisema kuendekezwa suala hilo na Rais Kikwete kumechangia kushusha zake alizozipata mwaka 2005.
“Nilimkataa Rais Kikwete tangu mwaka 2005 kwa kujua sio kiongozi kwa ajili ya watu bali kiongozi ambaye ana udini katika kutawala wananchi, hivyo hata sasa naamini Rais ni wa dini ya Kiislaam kwa kuonyesha katika uteuzi wa wabunge alioufanya,” alisema.
Alisema katika uteuzi huo, Kikwete amewatea Waislam pekee ambao ni Zakia Meghji, Shamsi Vuai Nahodha na Profesa Makame Mnyaa Mbarawa.
Alisema kuwa suala la udini kwa Rais Kikwete ni kutekeleza maazimio ya OIC kuteketeza Ukristo nchini kwa kutumia wadhifa wake wa uongozi kama inavyoagiza Katiba ya OIC na kuweka Mahakama ya Kadhi.
0 comments:
Post a Comment