
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa amekosoa uteuzi wa Baraza la Mawaziri kwa kusema kuna wizara zinazoundwa ili kufurahisha watu fulani.
Dk. Slaa amesema. Wizara hizo hazina kazi za msingi, hivyo ilitakiwa zipunguzwe ili kupunguza gharama za Serikali.Amesema, kuundwa Baraza kubwa ni kuendeleza ufisadi ndani ya Serikali, kwa kuwa gharama kubwa itatumika kulihudumia kuliko kuwapelekea wananchi maendeleo.
Ametoa mfano wa Wizara ya Utawala Bora, akidai haina kazi yoyote ya msingi zaidi ya kuchapisha kijitabu kimoja kinachoonesha idadi ya kesi za rushwa nchini.
“Fikiria kuna wizara iliundwa akapewa Kingunge Ngombale-Mwiru, ikaitwa inajishughulisha na Mambo ya Siasa, lakini mpaka anaondoka madarakani, wizara hiyo haikuwahi kuonana na chama chochote cha siasa, sasa kuna wizara za aina hiyo nyingi kwa kufurahisha watu tu,” amedai mwanasiasa huyo.
Endelea kusoma habari hii.....
0 comments:
Post a Comment